Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (KWANZA KUSHOTO) akimkaribisha
mzazi aliyefika katika banda la chuo hicho ili kupata maelezo ya nanma
ya kujiunga na Chuo katika maonesho ya vyuo vikuu Mnazi mmoja Jijini Dar
es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (KWANZA KULIA) akiteta jambo na
Afisa habari wa Chuo hicho Ngaja Mchele wakati wa hafla ya ufunguzi
rasmi wa maonesho hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (aliyevaa suti)akisalimiana na
baadhi ya wawakilishi wa vyuo vilivyohudhuria katika maonesho hayo
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (aliyevaa suti)akiwa na Afisa
habari wa Chuo hicho wakiteta jambo katika maonesho ya Vyuo Vikuu maeneo
ya viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam
…………………………………………………………………………….
Chuo kikuu cha Waislamu cha
Morogoro kinataraji kuongeza kozi mbalimbali zinazoendana na mahitaji ya
jamii katika Nyanja mbalimbali ili kuhakikisha kinatoa wanafunzi wenye
weledi katika kukuza uchumi wa Taifa.
Hayo yamebainishwa leo na Makamu Mkuu wa Chuo hicho upande wa Utawala na
fedha Profesa Musa Asad alipotembelea maonesho ya 15 ya Vyuo vikuu nchini yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
fedha Profesa Musa Asad alipotembelea maonesho ya 15 ya Vyuo vikuu nchini yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Profesa Asadi amesema Chuo kimeangalia mahitaji ya Taifa katika
wakati huu ambao nchi ipo katika uchumi wa kati hivyo inahitaji
wataalamu wa fani mbalimbali ambazo zitakuwa sababu ya kukuza uchumi
kuelekea viwango vya juu.
Profesa Asad ameongezea kuwa kozi za Afya ni miongoni mwa kozi
zitakazoongezwa kutoka zile zilizopo sasa ili kuongeza wataalamu zaidi
katika fani hiyo lengo likiwa kumsaidia Mtanzania kuondokana na uhitaji
wa kusafiri nje kupata matibabu.
Pamoja na hayo Profesa Asad ameendelea kusema kuwa Chuo hicho
kipo katika mkakati wa kuwa kinara katika utunzaji wa mazingira ambapo
kuna mpango maalumu wa kugeuza taka zinazozalishwa chuoni hapo kuwa
mbolea itakayotuika kukuzia miche itakayooteshwa na chuo hicho.
No comments :
Post a Comment