
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anasikitika kutangaza kifo cha Afisa
Mkuu Brigedia Jenerali Nelson Hosea Msanja (mstaafu)
Brigedia Jenerali Msanja
(Mstaafu) aliaga dunia tarehe 10 Septemba, 2020 katika
Hospitali ya Life Groenkloof nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Marehemu alizaliwa tarehe 01
Julai, 1958 katika Kijiji cha Utemini, Tarafa ya Utemini, Wilaya ya
Singida Mkoa wa Singida. Alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania tarehe 19 Disemba 1979.
Katika utumishi wake Jeshini
marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Kaimu Mkuu wa Tawi
la Ukaguzi Jeshini (2013 – 2015); Kamishna wa Utafiti na
Maendeleo ya Jeshi Wizara ya Ulinzi na JKT (2015-2017); Kaimu Mkuu wa
Tawi la Uhandisi na Logistiki Jeshini (2017) na Mwambata Jeshi nchini
Afrika Kusini hadi alipostaafu kwa heshima tarehe 30 Juni 2020.
Brigedia Jenerali Msanja
(Mstaafu) alitunukiwa medali zifuatazo katika miaka 40 na miezi sita ya
utumishi wake: Vita ya Kagera; Miaka 20 ya JWTZ; Utumishi mrefu; Miaka
40 ya JWTZ; Utumishi Uliotukuka; Nishani ya Comoro; Miaka 50 ya Uhuru;
Miaka 50 ya Muungano na Miaka 50 ya JWTZ.
Mwili wa Marehemu utawasili
nchini kwa ndege ya JWTZ tarehe 17 Septemba, 2020 na kwenda kuhifadhiwa
katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo (521KJ).
-2-
Heshima za mwisho kwa marehemu
zitatolewa katika eneo la kuagia la Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo
tarehe 18 Septemba, 2020. Kuanzia saa 3:00 asubuhi na mazishi
yatafanyika tarehe 19 Septemba, 2020 nyumbani kwake Chanika
Mwisho Jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.
No comments :
Post a Comment