Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa zoezi
la ugawaji wa mbolea bure kwa wakulima wa Mkoa wa Songwe katika msimu wa
kilimo 2020/2021 leo tarehe 16 Februari 2020. (Picha Zote Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu
ya wakulima wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga
wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa mbolea bure kwa
wakulima wa Mkoa wa Songwe katika msimu wa kilimo 2020/2021 leo tarehe
16 Februari 2020.
Sehemu
ya wakulima wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga
wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa mbolea bure kwa
wakulima wa Mkoa wa Songwe katika msimu wa kilimo 2020/2021 leo tarehe
16 Februari 2020.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa zoezi
la ugawaji wa mbolea bure kwa wakulima wa Mkoa wa Songwe katika msimu wa
kilimo 2020/2021 leo tarehe 16 Februari 2020.
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia
Jenerali Nicodemas Mwangela pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe John
Palindo wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa mbolea bure
kwa wakulima wa Mkoa wa Songwe katika msimu wa kilimo 2020/2021 leo
tarehe 16 Februari 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga amezindua zoezi muhimu la
ugawaji wa mbolea
bure kwa wakulima wa Mkoa wa Songwe ili waweze kuitumia katika msimu wa
kilimo 2020/2021.
Amesema
kuwa mkoa wa Songwe umekuwa ukizalisha chakula kwa kiasi kikubwa huku
ukishika nafasi ya tatu kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya Nafaka
baada ya Ruvuma na Rukwa.
Pia
amewapongeza Wanasongwe kwa kuitikia wito wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wa kufanya kazi kwa
bidii ili kuongeza tija kwenye mazao ya kilimo ikiwa ni pamoja na
matumizi bora ya mbolea.
Hasunga
amesema kuwa msaada huo wa kampuni ya YARA ni chachu kubwa ya kuendelea
kuzalisha kwa wingi zaidi ili kujihakikishia usalama wa chakula na pia
kurahisisha uwezo wa kuuza chakula mdani na nje ya nchi.
Ameataka watanzania kutembea kifua mbele kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inawajali watanzania wote.
Hasunga
ameeleza kuwa, Nchi nyingi za jirani zinaitegemea Tanzania kwa chakula
kwa hivyo mbolea hiyo iliyotolewa kwa wakulima itasaidia kuzalisha zaidi
na kuuza zaidi katika nchi hizo.
“Hii
itawaongezea kipato lakini Serikali pia itakusanya kodi nyingi zaidi
kutokana na mauzo ya mazao haya ili kuweza kutekeleza miradi zaidi ya
maendeleo” Amesisitiza Waziri Hasunga
Msaada
huo una thamani ya Bilioni 16.5 wenye uzito wa MT12,500 hivyo Waziri
Hasunga ametoa mwito kwa wakulima kuitumia vyema mbolea hiyo ili waweze
kuwa na matokeo makubwa yatakayoongeza tija na Pato la Taifa.
Pamoja
na mbolea hio ya bure, wakulima pia watapata ushauri wa bure kutoka
YARA kuhusu namna ya kutumia mbinu za kisasa za kidijitali za kuongeza
uzalishaji ili kuhakikisha Mkoa wa Songwe unazalisha chakula cha
kutosha, ili wakulima waweze kujiongezea kipato na pia kuhakikisha afya
bora kupitia uzalishaji wa vyakula vyenye rutuba sahihi.
Hasunga
amewataka wakulima kupitia vyama vya msingi kuhakikisha msaada huo
unatumika vizuri ili matokeo yake yawe mazuri na kwa wakati. “Tusisite
kuomba ushauri kutoka YARA pale ambapo tunakwama, kwani wamejitolea
kutoa ushauri wa kitaalamu bure jambo amabalo ni muhimu sana na la
kuigwa” Amesema Waziri Hasunga.
No comments :
Post a Comment