Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) wakimsikiliza mgeni rasmi
Dkt. Ayoub Kibao aliyemwakilisha mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
wakati wa uzinduzi wa kliniki maalum ya wagonjwa wenye sikoseli ambao
pia wanakabiliwa na magonjwa ya moyo iliyoko katika Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
(MUHAS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa
kliniki maalum ya wagonjwa wenye sikoseli ambao pia wanakabiliwa na
magonjwa ya moyo iliyoko katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini
Dar ess Salaam.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam Dkt. Ayoub Kibao, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkuu wa Idara ya Tiba
wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) ambaye pia ni Mkuu
wa Utafiti katika programu ya sikoseli na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya
Figo, Paschal Ruggajo wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kliniki
maalum ya wagonjwa wenye sikoseli ambao pia wanakabiliwa na magonjwa ya
moyo iliyoko katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar ess
Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza jambo na
Dkt. Emmanuel Balandya ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Masomo ya Elimu
ya juu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Mkuu wa
Idara ya Tiba wa MUHAS ambaye pia ni Mkuu wa Utafiti katika programu ya
sikoseli na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Paschal Ruggajo mara
baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa kliniki maalum ya wagonjwa wenye
sikoseli ambao pia wanakabiliwa na magonjwa ya moyo iliyoko katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar ess Salaam.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam Dkt. Ayoub Kibao akizungumza jambo wakati akikagua
chumba cha kufanyia kipimo cha kuangalia umeme wa moyo
(Electrocardiogram) katika kliniki maalum ya wagonjwa wenye sikoseli
ambao pia wanakabiliwa na magonjwa ya moyo iliyoko katika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar ess Salaam.
********************************
Na Mwandishi Maalum – Dar es Salaam
16/09/2020
Kliniki maalum kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa sikoseli ambapo
wanaokabiliwa pia na magonjwa ya moyo imeanzishwa katika Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI).
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Pro.
Mohamed Janabi amesema wameshirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kupitia Programu yake ya Sikoseli.
Prof.
Janabi, amesema juhudi za kuianzisha kliniki hiyo zilianza takribani
miaka miwili iliyopita na kwamba inalenga kuboresha huduma za matibabu
ya wagonjwa hao.
Amesema
JKCI kila wiki huwa tunawaona kwenye kliniki zetu na kwamba kabla ya
kuanzisha kliniki hiyo ilimlazimu mgonjwa anayehudhuria kliniki ya
sikoseli anayegundulika kuwa na shida ya moyo, kuelekezwa JKCI ili
kwenda kupangiwa tarehe ya kuanza kliniki ya moyo.
“Tukaona
ni adha kubwa kwao, maana yake analazimika kuhudhuria kliniki mbili.
Sikoseli ni ugonjwa wa damu, mtu mwenye sikoseli yupo kwenye uwezekano
wa kupata magonjwa ya moyo, japo si wote ambao huishia kupata magonjwa
ya moyo, lakini mtu akiwa na ugonjwa wa moyo hawezi kupata sikoseli,”
amebainisha.
Ameongeza
“Kwa sababu sikoseli wenyewe ni ugonjwa ambao mtu anaupata kwa kurithi
vinasaba kutoka kwa wazazi, uhusiano wake na magonjwa ya moyo ni kwamba
sikoseli ni tatizo la kwenye damu, wagonjwa wa sikoseli hukabiliwa na
upungufu wa damu, hali hii inaweza kuleta athari kwenye moyo na hata
viungo vingine vya mwili.
“Kunapokuwa na upungufu wa damu, maana yake mwili unakuwa na damu chache lakini moyo bado hulazimika kupiga zaidi ili kuisukuma.
“Sasa
neno ‘circle’ limetokana na vile visu vya kunolea mpunga (mundu), yaani
zile chembe chembe za damu huwa hazipo kwenye muundo wa kawaida wa
duara, zinapokuwa kwenye umbo la mundu ‘zina-tendency’ (tabia) ya
kugandisha damu.
“Damu
inapoganda inaweza kuziba kuziba mishipa ya damu na hali hiyo huwa
haichagui itokee wapi, ikiganda kwenye mishipa iliyopo kwenye moyo ndipo
uhusiano na magonjwa ya moyo unapotokea, wengne hupata pia ugonjwa wa
kiharusi,” amebainisha.
Ameongeza
“Zile changamoto zinazotokea kwenye damu ndiyo zinaleta athari kwenye
moyo, kwa hiyo sikoseli ndiyo inasababisha ugonjwa wa moyo, lakini mnoyo
wenyewe hauwezi kusababisha sikoseli.
“Hivyo,
wataalamu tulishauriana na kukubaliana kuanzisha kliniki hii maalum kwa
wagonjwa hawa kwa sababu ni magonjwa yanayoingiliana, mgonjwa
atakapokuja ataweza kuonwa na madaktari wa magonjwa yote mawili kwa
wakati mmoja,” amesisitiza.
Amebainisha
kutokuwa na kliniki ya wagonjwa wa sikoseli kwa upande wa watoto pia
watu wazima na kwamba watafanyiwa vipimo vyote vya moyo na damu na
kupatiwa dawa kadri itakavyoshauriwa.
“Tumeanza
na sikoseli, siku zijazo dhumuni letu ni kufikia hatua ya kuanzisha
kliniki moja kwa magonjwa yanayoingiliana kwa mfano moyo na figo, au
moyo na kisukari, kumrahisishia mgonjwa kuhudumiwa na kumuepushia adha
ya kukimbizana huku na kule, kufuata huduma,” amesema.
Mkuu
wa Idara ya Tiba wa Muhas ambaye pia ni Mkuu wa Utafiti wa Muhas katika
programu ya sikoseli na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Paschal
Ruggajo amesema kliniki hiyo itawasaidia pia wataalamu kujadiliana na
kufanya tafiti zaidi ili kuimarisha na kuboresha tiba za wagonjwa wa
sikoseli.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wagonjwa wa Sikoseli Nchini, Arafa Said amepongeza hatua
hiyo na kubainisha kwamba gharama za matibabu bado ni changamoto kubwa
inayowakabili.
“Wengi
wetu hawana bima ya afya na wapo wanaokata tamaa na kuacha kuhudhuria
kliniki, tunaendelea kujitahidi kutafuta wafadhili, ili kuwasaidia,”
amesema.
Akizungumza,
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Ayoub Kibao
amewahamasisha watanzania kukata bima ya afya kwani inasaidia kupunguza
mzigo wa gharama za matibabu.
“Takwimu
zinaonesha nchini kila mwaka watoto 8000 hadi 11,000 huzaliwa na
ugonjwa huu, nawashauri hasa vijana wanaotaka kuingia kwenye ndoa,
wapime ili kujua iwapo wamebeba vinasaba vya ugonjwa huu ama la,”
ameshauri.
No comments :
Post a Comment