Mjumbe
wa mtandao wa kupingana na udhalilishaji Mkoa wa kaskazini Unguja Kamu
Vuai Khamis akiwasilisha ripoti fupi dhdi baada ya kufanyika kwa mafunzo
ya kupambana na matukio ya udhalilishaji katika mkoa wa kaskazini
Unguja.
************************************
Chama cha
Waaandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha
udhalilishaji wanawake na watoto unamalizika Zanzibar kimewapa mafunzo
ya kupambana na matendo hayo wanajamii wapatao 1972 katika mkoa wa
kaskazini Unguja.
Mafunzo hayo
ambayo yameweza kuwanufainsha wanajamii wa mamakundi mbali mbali kutoka
shehia tofauti ndani ya mkoa huo kwa kutumia wanamtandao maalumu ambao
wamewezeshwa na Chama hicho katika utowaji wa elimu dhidi ya
udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
Akizungumza
katika uwasilishwaji wa taarifa baada ya kufanyika wa mafunzo hayo Afisa
ufuatiliaji na tathmini kutoka TAMWA-Zanzibar Mohamed Khatib alisema
utolewaji wa mafunzo hayo kwa jamii unalenga kuionesha jamii madhara ya
udhalilishaji kwa watoto ambapo anaamini kuwa jamii isipokua na uelewa
hwenda matendo hayo yakaendelea kusalia siku hadi siku.
Alisema
wameamua kutoa elimu hio kwa idadi kubwa ya watu kutoka katika makundi
mbali mbali ambayo yamekua katika mazingira hatarishi pia na kuna
ulazima wa kupatiwa elimu hio.
Hata hivyo
Afisa huyo alisema kuwa miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo ni pamoja
na wanafunzi waliopo vyuoni ikiwemo chuo cha amali mkokotoni pamoja na
kambi za JKU ambapo kwa kiasi kikubwa wanaonekana kuwa katika mazingira
hatarishi kufuatia mchanganyiko wao na jamii tofauti.
Pamoja na
hayo Afisa huyo aliwataka wanamtandao wa kupambana na udhalilishaji wa
kijinsia mkoa wa kaskazini Unguja kuhakikisha wanafanya kazi zao bila ya
kuchoka kwa maslahi ya jamii dhidi ya matendo hayo maovu.
‘’Ni lazima
muwe na utaratibu wa kuitazama jamii kwa jicho la mbali na ikiwezekana
elimu iliotolewa iwafikie wengi zaidi hata wale wasiokuepo kwenye
mikutano yetu’’aliongezea.
Akiwasilisha
ripoti ya utafiti mdogo uliofanywa na wanamtandao huo wa kaskazini
Unguja Bi Kamu Vuai Khamis alisema zipo changamoto mbali mbali ambazo
zinaendelea kuwakabili katika kupambana na vita ya udhalilishaji.
Akitaja
changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya wanajamii kutokua tayari kutoa
mashirikiano kwa wanamtandao kwa lengo la kuibua kesi za udhalilishaji
ambazo miongoni mwao ni watoto wao wanaofanyiwa.
‘’Kwa mfano
hivi sasa katika moja ya shehia mkoa wa kaskazini Unguja mama mtoto
amediriki kuficha taarifa za mtoto wake aliebakwa na kuamua kumpa dawa
za kiswahili akiamini anaweza kupoa na hadi sasa bado mtoto huyo
anaedelea na maumivu’’alisema.
Akizungumzia
kuhusu hali halisi ilivyo dhidi ya matukio hayo ya udhalilishaji alisema
kwa kipindi cha miezi miwili iliopita jumla ya kesi nane zimeripotiwa
huku saba kati ya hizo zinaendelea na ufuatiliaji na moja imeibuliwa kwa
hatua ya awali.
Kwa upande
wake Bi Hadia Ali Makame kutoka mkoa wa kaskazini Unguja ambae pia ni
miongoni mwa wanamtandao wa kupinga matendo ya udhalilishaji alisema
licha ya elimu kubwa inayoendelea kutolewa lakini bado kuna changamoto
ikiwemo muitikio mdogo kwa baadhi ya wanajamii.
No comments :
Post a Comment