Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi
akimfafanulia jambo Balozi wa Poland hapa nchini, Balozi Krzysztof
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Kabudi
akimkabidhi Balozi wa Italia nchini Balozi Roberto Mengoni vitabu vya
sheria ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi na miongozo mbalimbali
inayohusu masuala ya uchaguzi.

Balozi
wa Umoja wa Ulaya Balozi Manfred Fanti akimuelezea jambo Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John
Kabudi walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
*************************
Nchi 15 kupitia Balozi zao hapa
nchini zimeruhusiwa kuleta waangalizi wa Kimataifa katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba, 2020 baada ya Balozi hizo
kuwasilisha maombi na kufuata taratibu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Umoja wa Ulaya Balozi
Manfred Fanti na kuongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu kwa mara ya kwanza
umekuwa tofauti na miaka iliyopita kwa kuwa unafanyika kwa kugharamiwa
na fedha za ndani badala ya wahisani jambo ambalo baadhi ya watu
walianza kuhofia kutokuwepo kwa waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na
“Huu ni uchaguzi mkuu ambao kwa
mara ya kwanza kwa asilimia 100 tunaugharamia sisi wenyewe kama Serikali
ya Tanzania, utaratibu wa uchaguzi chini ya sheria ya uchaguzi na chini
ya utaratibu wa Kimataifa huwa tunakuwa na waangalizi wa uchaguzi na
mwaka huu nchi hizo 15 kupitia balozi zao zimepata kibali mara baada ya
kufuata taratibu za kuomba kuleta waangalizi wa uchaguzi mkuu,” Amesema
Prof. Kabudi
Mbali na Balozi wa Umoja wa Ulaya
pia Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia
hapa nchini Balozi Roberto Mengoni na baadae Balozi wa Poland Balozi
Krzysztof Buzalski ambapo amewakabidhi vitabu vya sheria ya uchaguzi na
kanuni za uchaguzi na miongozo mbalimbali inayohusu masuala ya uchaguzi
ili kuwapa fursa ya kufahamu namna uchaguzi unavyoendeshwa hapa nchini
hasusani baada ya uwepo wa malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya
upinzani juu ya kuenguliwa kwa wagombea wao.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Balozi Manfred Fanti amesema Nchi za Umoja huo zimekuwa zikifuatilia kwa karibu mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu zinavyoendelea hapa nchini ambapo mpaka sasa wanaridhishwa na kampeni zinavyofanyika kwa uhuru na amani na sasa wanajiandaa na zoezi la uangalizi wa uchaguzi huo.
Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Roberto Mengoni amesema amevutiwa na namna vyombo vya habari vimekuwa vikitoa nafasi kwa wagombea wote kwa uhuru na bila ya ubaguzi na kupongeza namna Watanzania wanavyojitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea mbali na tishio la corona na kwamba ana imani kuwa Kiongozi atakayechaguliwa atakuwa ametokana na utashi wa wananchi.
Mbali na masuala ya uchaguzi mkuu, Waziri Kabudi na Mabalozi hao wamejadili pia masuala ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia,maendeleo ya kiuchumi,biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,maji na miundombinu.

No comments :
Post a Comment