
Aliyepo kushoto ni
Mtendaji wa kata ya Kati, Suleiman Kikingo na wa pili yake Ni Mkurugenzi
wa Bodi ya maji bonde la Pangani,Segule Segule akizungumza katika kikao
kazi hicho kilichowashirikisha watendaji wa mitaa na kata katika jiji
la Arusha

Baadhi ya watendaji
wa mitaa na kata katika jiji la Arusha wakiwa katika kikao Cha kujadili
changamoto za usimamizi wa rasilimali za maji katika jiji la Arusha
kilichoandaliwa na Bodi ya maji bonde la Pangani kilichofanywa mjini
hapa.(Happy Lazaro)

Baadhi ya watendaji
wa mitaa na kata katika jiji la Arusha wakiwa katika kikao kazi Kati ya
bonde la Pangani katika kujadili changamoto za usimamizi wa rasilimali
za maji katika jiji la Arusha
……………………………………………………………………
Happy Lazaro,Arusha.
Mkurugenzi wa maji
bonde la Pangani Segule Segule amesema kuwa, wapo katika mchakato wa
kubaini na kuvifuatilia visima vyote ambavyo vimechimbwa pasipo kufuata
taratibu na Sheria za uchimbaji.
Ameyasema hayo leo
wakati akizungumza katika kikao kazi Kati ya bonde la Pangani na
watendaji wa mitaa na kata katika jiji la Arusha ili kujadili changamoto
za usimamizi wa rasilimali za maji katika jiji la Arusha .
Segule alisema kuwa,
kumekuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria unaofanywa na wananchi katika
shughuli nzima za uchimbaji wa visima ambapo asilimia kubwa ya wananchi
wamekuwa wakichimba kiholela bila kufuata sheria zilizopo .
Alisema kuwa ,ni
wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kuwa wanafuata sheria katika
uchimbaji wa visima vya maji ikiwa ni pamoja na kupata vibali vya
uchimbaji kutoka mamlaka husika .
Segule amesema
visima takribani 300 Bado havijatambulika hivyo wanafanya juhudi za
kuzibaini kupitia baadhi ya kata kwa kufanya ufuatiliaji kwa vile
visima vilivyochimbwa pasipo kufuata taratibu na sheria katika
uchimbaji.
Akimwakilisha Mkuu wa
wilaya ya Arusha katika kikao hicho ,Afisa Tawala wa wilaya ya Arusha
Nyangusi Nailiba amesema wilaya itafuatilia kwa ukaribu Jambo hilo na
kuwachukulia sheria wale wote wanaoenda kinyume na Taratibu za Miongozo
ya uchimbaji visima .
Naye Afisa usafi na
mazingira jiji la Arusha, James Lobikoki amesema kuwa, semina hiyo
imekuja muda muafaka kwani asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa hawana
uelewa wowote juu ya uchimbaji wa visima ambapo wengi wao wamekuwa
wakichimba kiholela tu.
Lobikoki amesema
kuwa,kupitia semina hiyo italeta manufaa makubwa na kuwepo kwa usimamizi
ulio Bora kwa watendaji wa mitaa na kata ambao watakuwa mabalozi wazuri
wa kusimamia kikamilifu uchimbaji huo Huku wakifuata sheria na kanuni
zilizopo.
Aliwataka wananchi wa
jiji la Arusha kuhakikisha wanatunza kikamilifu mazingira na kuepuka
uchimbaji wa visima hovyo ambao umekuwa haufuati sheria na kanuni za
uchimbaji.
Baadhi ya watendaji
wa kata wakizungumza katika kikao hicho ,Mtendaji wa kata ya Kati
halmashauri ya Arusha,Suleiman Kikingo amesema kuwa,kikao hicho
kimewafungua wao Kama watendaji ambapo wataenda kuwa mabalozi wazuri
katika maeneo yao kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kufuata sheria na
taratibu za uchimbaji wa visima hivyo.
No comments :
Post a Comment