Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Utalii, Philip Chitaunga akizungumza na Wadau wa Utalii
wanaotoa huduma za malazi kwa Wageni katika mikoa ya Arusha, Manyara na
Kilimanjaro kabla ya kuanza kutolewa kwa mafunzo ya usajili wa Wageni
kwenye mfumo wa MNRT PORTAL yanayofanyika kwa muda wa siku mbili
kuanzia leo mkoani Arusha.
Baadhi ya Wadau wa
Utalii kati ya 250 wanaotoa huduma za malazi kwa Wageni walioshiki
kutoka katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro wakifuatilia
mafunzo ya usajili Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL yanayoendelea
kufanyika kwa siku mbili kuanzia leo mkoani Arusha.
Muwezeshaji wa
Mafunzo ya usajili Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL, Kelvin Mtei
akitoa mafunzo kwa Wadau wanaotoa huduma za Malazi wa mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro na Manyara, Mfumo huo wa Kielektoniki utaanza kutumia Oktoba
1, mwaka huu kwa Watoa Huduma hiyo nchini kote
Afisa Utalii wa
Wizara ya Maliasili na Utalii,Neema Salum akimsajili Juliana Haniu
ambaye ni moja Washiriki wa mafunzo ya MNRT PORTAL yaliyotolewa na
Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha leo.
Muwezeshaji wa
Mafunzo ya usajili Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL , Kelvin Mtei
akiwasajili baadhi ya Wadau wa malazi walioshiriki mafunzo hayo leo
mkoani Arusha.

Afisa Utalii wa
Wizara ya Maliasili na Utalii Mwinyi Mbegu akimpa maelezo Shabani
Hamisi ya namna ya kusajili Wageni wataokuja kulala katika Hoteli yake
mara baada ya kupata mafunzo ya kusajili Wageni kwenye MNRT PORTAL
yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia jana yaliyomalizika leo
Jijini Arusha.
…………………………………………………………………………..
Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii imewatoa hofu Wamiliki wa Huduma za Malazi wa mikoa
ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara kuwa usajili wa Wageni kwenye mfumo wa
MNRT PORTAL utakaoanza kutumika nchini kote Oktoba 1, 2020 umelenga
kupata takwimu sahihi za Wageni zitakazosaidia katika kuboresha sekta
ya Utalii nchini na si vingunevyo.
Pia, Imesema Usajili
huo utalinda siri za Wageni na zitatumika kwa ajili ya matumizi ya
Serikali pekee na sio kwa maslahi binafsi.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga
alipokuwa akihitimisha mafunzo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili ya
usajili Wageni kwenye Mfumo wa MNRT PORTAL kwa Watoa Huduma za
Malazi zaidi ya 250 wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara
Amesema Usajili wa
Wageni katika Mfumo huo utahusisha Wageni wa ndani pamoja na Wageni
kutoka nje ya nchi ambapo lengo kuu ni kupata takwimu zitakazosaidia
kuboresha sera, mikakati na mbinu za kukuza utalii nchini.
Amesema Usajili huo
mbali ya kusaidia kujua idadi ya Watalii wa ndani bali utawasaidia hata
Wamiliki wa malazi hayo kuweka rekodi ya Wageni waliolala katika malazi
yao kwa kipindi chote ambacho anafanya biashara hiyo ya malazi.
Chitaunga amesema
katika sekta ya utalii mfumo huo umekuwa ukitumika sehemu nyingi Duniani
kama vile Uingereza, Marekani na Kanada na si kitu kipya
kilichoanzishwa hapa nchini.
Pia amesema mfumo huo
utasaidia kurahisisha kazi kwa Wamiliki wa malazi ambapo badala ya
kubeba karatasi na kwenda katika ofisi za Wizara ya Maliasili na utalii
kwa ajili ya kulipia leseni ataweza kutumia kompyuta yake akiwa ofisini
kwake kufanya usajili huo
Mkurugenzi huyo
amesema mfumo huo utakaonza kutumiwa na Watoa Huduma za malazi nchini
kote mwezi Oktoba 1, 2020 utahusisha hoteli, loji, nyumba za Wageni
pamoja na mahema ya watalii.
Ametaja vitambulisho
vitakavyotumika katika usajili huo kuwa ni Kitambulisho cha Taifa kwa
wageni ambao ni Watanzania na Pasi ya kusafiria kwa Wageni wa kutoka
nchi za nje.
Katika hatua
nyingine, Chitaunga amesema kuanza kutumika kwa Mfumo huo ni utekelezaji
wa takwa la kisheria linalomtaka kila Mmiliki wa Malazi kuanza kusajili
Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL.
Mbali na hiyo,
Chitaunga amesema matumizi ya mfumo huo utaifanya sekta ya Utalii kwenda
katika uchumi wa bluu utakaoiweka Tanzania katika mazigira bora ya
kibiashara
Naye Anne Sosteness
ambaye ni miongoni mwa Wamiliki wa Malazi katika mkoa wa Arusha
aliyeshiriki mafunzo hayo, Amesema mafunzo ni mazuri na ni salama kwa
mteja na mtoa huduma kwa ssbabu Mteja anatakiwa kuonesha kitambulisho
chaTaifa au pasi ya kusafiria ili aweze kusajiliwa.
Aidha, Amesema mfumo huo unapunguza matumizi ya karatasi ambayo ni rahisi kupotea na kuchanika.
No comments :
Post a Comment