Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughurikia Sera, uratibu na uwekezaji Dkt Dorothy
Mwaluko,akifungua kikao kazi na taasisi mbalimbali zinazoshughulikia
wawekezaji kutathmini sera za uwekezaji iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia
hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughurikia Sera,
uratibu na uwekezaji Dkt Dorothy Mwaluko,(hayupo pichani) alipokuwa
akifungua kikao kazi na taasisi mbalimbali zinazoshughulikia wawekezaji
kutathmini sera za uwekezaji iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na
Uwekezaji Mamlaka ya EP2 Bw. James Maziku,akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na taasisi mbalimbali
zinazoshughulikia wawekezaji kutathmini sera za uwekezaji iliyofanyika
leo jijini Dodoma.
Mtafiti wa sheria za uwekezaji
hapa nchini Dkt Saudin Mwakaje,akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na taasisi mbalimbali
zinazoshughulikia wawekezaji kutathmini sera za uwekezaji iliyofanyika
leo jijini Dodoma.
……………………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Taasisi
zinazokwamisha uwekezaji hapa nchini kwa kuwawekea mazingira magumu
wawekezaji kuwekeza hapa nchini zimetakiwa kjitathimini kabla ya
kuchukliwa hata na
serikali.
Kauli hiyo
imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughurikia Sera, uratibu na uwekezaji Dkt Dorothy Mwaluko wakati
akifungua kikao kazi na taasisi mbali mbali zinazoshughurikia wawekezaji
kutathmini sera za uwekezaji.
“ Bado kuna
taasisi ambazo zinakuwa kikwazo kwa wawekezaji kuwekaza hapa nchini kwa
kuwawekea mazingira magumu na kushindwa kuwekeza hapa nchini”, ameeleza
Dkt. Mwaluko.
Dkt. Mwaluko
amesisitiza kuwa wawekezaji hao wako getini hivyo ni wajibu wao
kuwafungulia milango wawekezaji kwani serikali na wao wanaongea lugha
moja sio kila taasisi inakuwa na sheria zake na haishauriki inapokuwa
inakinzana na nyingine
” Hivyo sio
mnaweka sheria ambayo hata wewe mwenyewe tukisema haya hamia huku
utekeleze hiyo sera na wewe unashindwa kuitekeleza kwa namna hiyo
tutakuwa hatuwawezeshi wawekezaji kuja kuwekeza” ameweka wazi Dkt
Mwaluko.
Lakini pia Dkt.
Mwaluko amesisitiza kuacha kuwachanganya wawekezaji kwa kutofautiana
katika sera na kuwataka wawe na sheria ambazo zitamuwezesha muwekezaji
kuja kuwekeza.
Kwa kuongezea
Dkt. Mwaluko amekumbushia kuwa taasisi hizo hazina uamuzi wa mwisho
katika kuamua sera hizo maamuzi yapo ngazi za juu za katika serikali.
Naye Mtafiti wa
sheria za uwekezaji hapa nchini Dkt Saudin Mwakaje amesema kuwa kikao
hicho kitasaidia kutathmini hali ya uwekezaji hapa nchini na changamoto
wanazozipata Taasisi hizo katika kutekeleza sera hizo.
Dkt Mwakaje
amesema watapitia sera mbalimbali na kuona kama zinaendana na hali ya
Sasa na kama kutakuwa na uhitaji watakuja na mapendekezo ya kuzibadili
sera hizo ili ziendane na wakati wa sasa.
No comments :
Post a Comment