Jeshi la Polisi Tanzania lilimkamata Saed Kubenea akiwa katika gari la abiria lenye namba ya usajili T. 645 DKR akitokea kwenye mpaka wa Tanzania na
Baada ya upekuzi wa Polisi, Kubenea
alikutwa, pamoja na vitu vingine, Dola za Marekani Elfu Nane (USD 8000),
Shilingi za Kenya Laki Nne Tisini na Moja Elfu Mia Saba (KES 491,700),
Shilingi za Kitanzania Elfu Sabini na Moja (TZS 71,000/-), tiketi ya
basi la Super Couch lenye namba ya usajili KCP 4230 ya tarehe 05/09/2020
kutoka Nairobi, Kenya kwenda Namanga, ‘Memorandum of Understanding’
kati ya Hali-Halisi (Tanzania) na Buni Media Limited (Kenya), Risiti ya
malipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited iliyopo Nairobi, Kenya
yenye jina la Kubenea, Saed Ahmed kama mgeni kuanzia tarehe 3/9/2020
hadi 5/9/2020.
Anatuhumiwa kuvuka Mpaka usio rasmi na
kuelekea Nairobi nchini Kenya na kisha kurejea nchini Tanzania bila
kutumia Mpaka rasmi mnamo tarehe 5/9/2020.
Pia, anatuhumiwa kuingiza nchini Fedha za Kigeni (foreign currency) bila
kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya Kanuni za the
Anti-Money Laundering (Cross – Border Declaration of Currency and Bearer
Negotiable Instruments) Regulations, 2016 zikisomwa pamoja na Kifungu
cha 28B(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia Utakasishaji wa Fedha Haramu, Na. 12
ya Mwaka 2006.
No comments :
Post a Comment