Monday, September 7, 2020

Waandishi waaswa kutoa taarifa sahihi kwa Jamii


Mratibu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Paradigm Initiative Afrika, Peter Mmbando   akizungumza na waandishi wa habari na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika mkutano wa  kujadili masuala ya habari katika mitandao ya jamii na internet ,jijini Dar es Salaam.
 Mwanasheria wa Shirika la Organsation for Peace and Consensus Building (OPCB)  Ice Erick akichangia mada  katika mkutano namna ya kufuata sheria katika uhabarishaji wa habari,jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji Serengeti Bytes  Kennedy Mmari akichangia mada katika mkutano namna ya kufuata sheria za katika kuhabarisha jamii katika masuala ya Mitandao 
 Baadhi ya wadau wakifatilia mada kwa njia ya mtandao
 Picha ya pamoja ya waandishi habari na mashirika yasiyo ya kiserikali mara baada ya kumaliizika mkutano kwa njia ya mtandao.

*Matumizi ya Mitandao ya Jamii, Internet yatakiwa kuwa salama katika upatikanaji wa habari

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAANDISHI wa habari  nchini wametakiwa kufuata taratibu za uandishi wa habari zilizowekwa ili kulinda haki za wananchi kupata taarifa hasa katika matumizi ya mitandao ya jamii pamoja na Internet .

Akizungumza na waandishi wa habari  katika mkutano uliokutanisha wadau kuangalia na kujadiliana namna ya  sheria ya mtandao kwa Tanzania  jijini Dar es Salaam Mratibu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Paradigm Initiative Afrika, Peter Mmbando  amesema kuwa  uhuru wa vyombo vya habari  na sheria katika matumizi ya mitandao  na internet ni kuangalia namna ya kusaidia kuboresha ufanisi,  bora ya  upashanaji wa  habari na  kufuata taratibu zilizowekwa katika kupasha habari  jamii zenye kuzingatia ukweli na uhakika.

“Rai kwa Wanahabari   kufuata taratibu ambazo zimewekwa na mamlaka husika ili kulinda haki za wananchi katika  kuwapasha habari,Habari zinatakiwa ziwe za kweli hazitakiwi ziwe  za kutengeneza kwani  mtu anapodanganya jamii kwa sauti/video anaharibu taratibu uliowekwa kisheria.”Amesema.

Aidha aliyaonya makundi ambayo hayajasomea mambo ya habari, wanatakiwa kuacha kutoa taarifa ambazo hazina ukweli na kupotosha umma ni kuharibu utaratibu za mamlaka.

Kwa upande wake Ice Erick kutoka shirika  masuala ya umoja, Amani na maendeleo(OPCB), alisema kupitia mkutano huo wamejifunz amambo mengi yanayo husu matumizi sahihi ya mitandao na kuongeza kuwa changamoto za matumizi ya kimtandao ni jukumu lao  kuhakikisha watu ambao wanaweza kupata maafa kutokana na matumizi yasiyosahihi.

“Nadhani  katika matumizi ya mtandao  ni kuna umhimu wa  kuchukua hatua nzuri kwa sasa kuiga mfano kwa nchi zingine kama jambo litakuwa na matokeo mazuri kutoka nchi zingine kuweza kulinda uhuru wa matumizi ya mtandao.”Amesema.

Hata hivyo mmoja wa mshiriki wa mkutano huo, Kenedy Mmari alisema majadiliano hayo  muhimu hasa katika kushirikisha wadau katika michakato mbalimbali ya uundaji wa sera na sharia inayosimamia sekta mbalimbali ikiwemo  mawasiliano ya kimtandao na vyombo vya habari.

“Katika miaka ya hivi karibuni sheria nyingi zenye mlengo mzuri  zinazingatia habari sahihi mtandaoni, usimamizi mzuri wa mtandaoni lakini sababau za msingi kunapokuwa hakuna msimamizi wa habari za ukweli inaleta athari.”Alisema.

No comments :

Post a Comment