Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini
kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa India nchini Tanzani. Pembeni
yake kulia ni Balozi wa India nchini Mhe. Shri Sanjiv Kohli
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa India nchini
Tanzania
………………………………………………………………………..
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi
na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
wamesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa India nchini kufuatia kifo
cha Rais mstaafu wa Taifa hilo
Shri Pranab Mukherjee kilichotokea tarehe
31 Agosti 2020.
Akizungumza mara
baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi ubalozi wa India
nchini, Jijini Dar es Salaam Prof. Kabudi ametoa pole kwa wananchi wote
wa India na kuwasihi kuendelea kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu
wa msiba wa kiongozi wao mstaafu.
“Kusaini
kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na
undugu wetu na ndugu zetu wa India. Kifo cha Rais Shri Pranab Mukherjee
kinawahusu pia watanzania kwa sababu Tanzania na India zina uhusiano
mzuri, imara na wa muda mrefu ulianzishwa na baba wa Taifa Mwl. Julias
Nyerere pamoja na Mahatma Gandhi,” amesema Prof. Kabudi
Rais Shri
Pranab Mukherjee ni miongoni mwa viongozi wa zamani wa India waliowahi
kufanya kazi katika Serikali ya Waziri Mkuu wa Zamani Indira Gandhi
aliyewahi kukabidhiwa nyadhifa mbali mbali ikiwemo Waziri katika Sekta
tofauti.
No comments :
Post a Comment