Na Amiri Kilagalila, Njombe
SERIKALI Wilayani Njombe imeongeza muda wa siku nne kuanzia leo za
kutuma maombi kwa ajili ya kujiunga na nafasi za jeshi la kujenga Taifa
(JKT) kutokana na vijana kutojitokeza kwa wingi mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema zoezi hilo lilitakiwa
kukamilika septemba 9 mwaka huu na kutokana na idadi ndogo ya vijana
waliokwenda kuomba, serikali imeongeza muda huo wa siku nne hadi tarehe
11.
“Tarehe yetu ya mwisho ya kupokea tulikuwa tumepanga iwe tarehe 9 saa
kumi jioni ambayo ni kesho,lakini mimi nimefungua na nitaendelea
kupokea majina ya waombaji wote na vikao vyangu nitafunga rasmi tarehe
11”alisema Ruth Msafiri.
Aidha Bi.Msafiri amesema vijana wenye sifa ya kujiunga na JKT ni
wenye elimu ya darasa la saba hadi chuo kikuu ambapo vijana 130
wanahitajika kujiunga na jeshi hilo.
“Kwa kuwa lengo ni kupata vijana wa kutosha kupata fani na stadi
mbali mbali za maisha,hii inahusisha madarasa yote kwa maana elimu ya
msingi,sekondari,kidato cha sita, cheti, lakini pia hata wa chuo
kikuu”aliongeza DC Msafiri.
B.Msafiri ametumia fursa hiyo kukemea tabia za baadhi ya watu
wanaotaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia zoezi hilo
kinyume na sheria ambapo kwa atakaye bainika hatua kali zitachukuliwa.
“Hizi nafasi hazitolewa kwa upendeleo wa aina yeyote,wewe ukitoa
rushwa utakuwa umeumizwa,mimi sitoi hiz nafasi kwa upendeleo kwasababu
sio za mfukoni ila tunakwenda nazo kwa sifa”alisema Ruth Msafiri
Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya vijana mjini Njombe wamesema
wanatambua kuwepo umuhimu wa kujiunga na JKT ikiwemo kujengewa uzalendo
na kulilinda Taifa.
No comments :
Post a Comment