**************************************
Na Karimu Meshack, Sumbawanga
Hayo yamesemwa na
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule alipotembelewa na Kamati
ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari ofisini kwake
leo.
Dkt. Haule ametaja
mafanikio yaliyofanywa na Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. John Joseph
Pombe Magufuli katika Sekta za Afya, Elimu, Barabara, Umeme, Maji na
upatikanaji haki kwa wakati kuwa ni kichocheo cha ujenzi wa amani na
utulivu hapa nchini.
“Huduma za jamii kama
maji, elimu, umeme, afya, usafiri na usafirishaji ni haki ya msingi ya
kila mwananchi. Naipongeza Serikali yangu chini ya Rais wetu mpendwa
Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuyapa kipaumbele masuala haya
muhimu katika ujenzi wa amani na uchumi wa Taifa kwa kwa ujumla” amesema
Dkt Haule.
Mwananchi akipata
haki ya maendeleo kwa kuboreshewa na kusogezewa karibu huduma za jamii
na nyingine hawezi kujihusisha na migogoro yoyote katika jamii kwani
akili yake inakuwa imetulia, hivyo kujielekeza katika kufanya shughuli
za maendeleo na kujipatia kipato, ameongeza Dkt. Haule.
Hata hivyo, Dkt.
Haule ameiomba Serikali kuendelea kuweka mkazo na juhudi katika
kuhakikisha huduma za jamii zinawafikia wananchi wote katika maeneo yao
kama inavyojieleza katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya
Mwaka 2020/2025.
Kwa upende wake
Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya
Kimbari Bwn. Miraji Magai Maira wakati akimshukuru Mkuu huyo wa Wilaya
ya Sumbawanga amesema wanalazimika kufika kwa wananchi na kukutana na
makundi mbalimbali ya vinaja, wafugaji, wakulima, Walemavu, viongozi wa
Mira na viongozi wa dini kwasababu huko ndiko migogoro inakoanzia na
isiposhughulikiwa kwa wakati huhatarisha amani ya nchi.
Kamati ya Kitaifa ya
Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari iliyoanzishwa Februari, 2012
chini ya itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na kuridhiwa na serikali
ya Tanzania kupitia Mkataba wa nchi za Maziwa Makuu wa Usalama, Utulivu
na Maendeleo itaendelea na mkakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya
msingi ya kujenga na kudumisha amani na utengamano kwa kufanya vikao vya
ujenzi wa amani kwa siku mbili katika mkoa wa Rukwa, Wilaya ya
Sumbawanga na baadae kumalizia vikao hivyo mkoani Morogoro.
No comments :
Post a Comment