Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zenais Ngowi akitoa
maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu ya uelewa wa magonjwa ya moyo kwa
mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo katika viwanja vya Mbagala
Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo
Taasisi hiyo ilitoa bila malipo huduma za upimaji, matibabu na ushauri
wa magonjwa ya moyo.
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Steven Lugu akimpima
shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa
ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika viwanja vya
Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo
wananchi 103 walifika katika banda hilo na kupewa huduma za ushauri na
upimaji wa magonjwa ya moyo.
Wananchi
waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika
viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop
Jawabu wakipata huduma mbalimbali za upimaji, matibabu na ushauri wa
magonjwa ya moyo ambapo watu 103 walifika katika banda hilo na kupewa
bila malipo huduma za ushauri na upimaji wa magonjwa ya moyo.
Afisa
Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akimpa
mwananchi elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo wakati wa jukwaa la One
Stop Jawabu lililofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani
Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo Taasisi hiyo ilitoa bila
malipo huduma za upimaji, matibabu na ushauri wa magonjwa ya moyo.
Picha na JKCI
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
21/09/2020
TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imewaibua watu 21 wenye matatizo
mbalimbali ya moyo, 18 wamekutwa na shinikizo la damu, walipochunguzwa
afya zao katika Viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kwenye
jukwaa la One Stop Jawabu.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI,
Samweli Rweyemamu alisema watu 16 kati ya 18 waliokutwa na shinikizo la
damu walikuwa hawajitambui kwamba wanakabiliwa na tatizo hilo.
“Hii
ni sawa na asilimia 18, yupo mmoja ambaye tumemkuta ana shinikizo la
damu 200 chini ya 110, ni mara yake ya kwanza amekuja kufanyiwa
uchunguzi, ni shinikizo ambalo lipo juu mno, tulidhani labda amepata
mshtuko alipofika hapa.
“Tulimtaka
akae kidogo apumzike, tukamfanyia tena uchunguzi na kukuta hali ikiwa
vile vile, endapo tusingemgundua alikuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza
maisha, tumempa rufaa kuja JKCI kwa matibabu,” amebainisha.
Dk.
Rweyemamu amesema mtu mmoja kati ya hao walifanyiwa uchunguzi amekutwa
na tatizo la kuziba kwa mshipa wa damu kwenye moyo, watu 10 wamekutwa na
kisukari.
“Watu
50 tuliwachunguza afya ya moyo kwa kutumia kipimo cha kuangalia jinsi
moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) na 53 tuliwafanyia
kipimo cha kuangalia umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG) wawili
kati ya hao tuliowachunguza tulikuta ‘valve’ zao za moyo zina tatizo,”
amebainisha.
Ameongeza
“Asilimia 50 ya watu wote tuliowachunguza wana uzito uliopitiliza, hii
ni hatari kwa afya ya mioyo yao. Watu 21 tumewapa rufaa kuja kwenye
Taasisi yetu kupitia Hospitali yao ya Mbagala Zakheem ili tuwafanyie
uchunguzi zaidi na kuwapa matibabu.
Amesema
ndani ya banda lao pamoja na uchunguzi wa afya ya moyo, vile vile
walitoa elimu ya lishe kwa wananchi hao ili waweze kulinda afya yao ya
moyo na mwili kwa ujumla.
“Tumewaelimisha
wazingatie ulaji unaofaa, waepuke vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi
nyingi, sukari nyingi na uvutaji wa sigara, ili kuepuka magonjwa yasiyo
ambukiza ikiwamo haya ya moyo.
“Tumewashauri
pia kukata bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata matibabu maana
gharama ni kubwa endapo ukiwa huna bima ya afya ni changamoto,”
amesema.
Wakizungumza
mara baada ya kupatiwa huduma katika banda la Taasisi hiyo wakazi wa
Mbagala ameipongeza Serikali na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Godwin Gondwe kwa kupeleka jukwaa hilo katika eneo hilo kwani wameweza
kufikiwa na kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo na hatimaye wengine
wamelutwa na matatizo na kupewa huduma ya matibabu.
“Kupitia
vyombo vya habari nilisikia siku ya leo wataalamu wa moyo watakuwepo
mahali hapa nikaamua kuja kupima afya yangu. Nimeweza kupima na kufahamu
hali yangu ikoje. Ninashukuru sana kwa huduma niliyoipata”,.
“Ninawashauri
wananchi wenzangu wanaposikia wataalamu kama hawa wanafanya upimaji
wajitokeze kwa wingi kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo
kutawasaidia kufahamu wanakabiliwa na matatizo gani ili waweze kupata
matibabu kwa wakati na kama hawana matatizo wataweza kujikinga”, alisema
Hamza Juma mkazi wa Chamazi.
No comments :
Post a Comment