Monday, September 21, 2020

GST YAPONGEZWA NA WAZIRI WA MADINI , DOTTO BITEKO

Waziri wa Madini Dotto Biteko aipongeza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania  (GST) juu ya tafiti za jiosayansi inazofanya katika sekta ya Madini.

Waziri Biteko ametoa pongezi hizo alipofika katika Banda la GST lililopo katika maonesho ya Tatu ya Tekinolojia na Uwekezaji katika sekta ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Akiwa katika Banda la GST na Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel waziri Biteko alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa sekta ya Madini nchini na kushauri kuwa bidhaa za sekta ya Madini  zinazozalishwa nchini ziuzwe ili kufuata utaratibu wa Mpango ushirikishwaji kwa Wazawa katika sekta ya Madini  nchini.
Katika maonesho haya GST kupitia Idara  zake imemuonesha na kumuueleza mafanikio mbalimbali ikiwapo  vyungu maalum vya kuyeyushia dhahabu na akapendekeza ufanyike utaratibu wa kuuza vyungu hivyo katika mgodi wa dhahabu wa STAMIGOLD
 

 

No comments :

Post a Comment