Monday, September 21, 2020

TBS YAENDELEA KUTOA ELIMU USINDIKIZAJI NA UHIFADHI KWA WAZALISHAJI NA WAUZAJI WA MAFUTA YA KULA NCHINI

Shirika la Viwango Tanzania TBS limeendelea na zoezi la utoaji Semina kwa wazalishaji, wasindikaji na wauzaji wa mafuta ya kula katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuwajengea uelewa juu ya kufahamu umuhimu wa bidhaa kukaguliwa na kukidhi ubora unaotakiwa.

TBS imeshawatembelea wafanyabiashara hao katika Mkoa wa Singida hasa kutokana na Mkoa huo kusifika kwa uzalishaji wa mafuta bora ya alizeti.

TBS imepanga kutembelea Mikoa ya Singida, Tabora na Dodoma.

Maafisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakiwa wameambatana na maafisa kutoka ofisi za Halmashauri ya manispaa ya Singida na Wizara ya Viwanda na Biashara, wakitoa elimu juu ya usindikaji na uhifadhi kwa muuzaji wa mafuta ya alizeti katika soko kuu mkoani Singida.

wakitoa elimu juu ya usindikaji na uhifadhi

 

No comments :

Post a Comment