Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (wa
kwanza kulia), akikata utepe kuzindua mnara wa mawasiliano wa Igando
mkoani Geita. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhandisi
Charles Kabeho na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula
akimsikiliza kwa makini Meneja Mipango Mtandao wa Shirika la Mawasiliano
Tanzania, Mhandisi Innocent Msasi akitoa maelezo kuhusu mnara wa
mawasiliano wa Naybilezi, Geita baada ya kuzinduliwa rasmi na katibu
Mkuu huyo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula
akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Chato, Denis Bandisa baada ya
kuzindua mnara wa mawasiliano wa Igando mkoani humo. Anayesikiliza kulia
ni Mkuu wam Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi
Charles Kabeho, akizungumza na wananchi wa Igando kabla ya kumkaribisha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (aliyevaa kilemba), kuzindua mnara wa
mawasiliano ya simu kijijini humo mkoani Geita
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt.
Zainabu Chaula (aliyevaa kilemba) kuhusu gharama za ujenzi wa mnara wa
mawasiliano wa Nyabilezi na Igando kabla ya uzinduzi wa minara hiyo
kijijini Igando mkoani Geita
Wananchi wa Kijiji cha Igando
kilichopo mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu
Chaula (hayupo pichani) akizungumza nao baada ya kuzindua mnara wa
mawasiliano kijijini humo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato,
Mhandisi Charles Kabeho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula
akimpatia Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho, vitabu
vyenye orodha ya maeneo ilikojengwa minara ya mawasiliano kwa kutumia
ruzuku ya Serikali iliyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchi
nzima
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula
(aliyevaa kilemba), akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Chato, Mhandisi Charles Kabeho (aliyesimama kulia) na wananchi wa Kijiji
cha Igando baada ya Katibu Mkuu huyo kuzindua mnara wa mawasiliano
kiijijini humo.
…………………………………………………………….
*Asema Mawasiliano ni uchumi, maendeleo, uwekezaji na huduma
*Atoa rai kwa wananchi kutumia mawasiliano kudumisha amani na mshikamano
Na Prisca Ulomi, WUUM, Chato
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt.Zainabu Chaula
amezindua minara miwili ya mawasiliano iliyopo kwenye kijiiji cha
Nyabilezi na Igando vilivyopo wilayani Chato mkoani Geita ili
kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano
Dkt. Chaula amesema kuwa ujenzi wa
minara hiyo umefanyika kwenye vijiji hivyo baada ya wananchi kuomba
huduma za mawasiliano na Serikali kujiridhisha kuwa mawasiliano hayapo
kwenye maeneo hayo na kuamua kujenga minara hiyo kwa kutumia ruzuku ya
Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambapo ujenzi
wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano
Ameongeza kuwa lengo la Serikali
ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano kwa kuwa
mawasiliano ni uchumi na Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa kujenga
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao ni sawa na barabara kuu kwa ajili
ya kupitisha ya uhakika na kwa wakati ambapo minara hiyo imeunganishwa
kwenye Mkongo huo ili kuweza kuwapatia wananchi huduma
Naye Katibu Tawala wa Mkoamwa
Geita, Denis Bandesi amesema kuwa miundombinu ya mawasiliano ambayo
imewekwa kwenye maeneo hayo itawasaidia wananchi kufanya mawasiliano na
kuendesha biashara zao ili kuhakikisha kuwa uchumi wa kati unamgusa
mwananchi pale alipo kwa maana uzalishaji atakaokuwa ameufanya atakuwa
na uhakika wapi apeleke biashara yake kwa maana ya uhakika wa bei nzuri
mahali soko lililopo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba amewataka wananchi
kuchangamkia fursa ya kuwa mawakala wa huduma za mawasiliano wa Shirika
hilo kwa kuwa TTCL inatoa kamisheni mara mbili ya kampuni nyingine za
mawasiliano na fedha inayopatikana inarudi Serikalini na ameomba
wananchi wailinde miundombinu hiyo kwa kuwa imetumia fedha za Serikali
kujengwa na ikiharibika wananchi watakosa mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhandisi
Charles Kabeho ameahidi kuwa atahakikisha miundombinu hiyo inalindwa ili
wananchi wanufaike na huduma za mawasiliano kwa kuwa hapo awali
hapakuwa na huduma za mawasiliano ila kwa sasa mtandao wa TTCL uko
vizuri na wananchi wanaweza kupiga simu ndani na nje ya Tanzania
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema kuwa UCSAF ina
jukumu la kupeleka mawasiliano vijijini ambapo mpaka sasa UCSAF ina
miradi ya ujenzi wa minara ya mawasiliano sehemu mbali mbali nchini
kwenye kata 998 ambapo hadi sasa ujenzi umekamilika kwenye kata 903
ambapo zaidi ya wananchi wapatao milioni tano wanapata huduma za
mawasiliano
No comments :
Post a Comment