Wafanyakazi Chuo Kikuu Mzumbe wakitoa Maelekezo kwa wanafunzi
waliofika Katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya vyuo
Vikuu yanayoendelea kufanyika Katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Ganka Nyamsogoro
akisisitiza jambo alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika
maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu
nchini(TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es
Salaam.
Wafanyakazi Chuo Kikuu Mzumbe wakifanya usahili katika maonesho ya 15
ya vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam kwa wiki moja.
BANDA
la Chuo Kikuu limekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 15 ya Vyuo
Vikuu yaliyoanza leo viwanja vya viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Hii ni kutokana na wingi wa programu na ubobevu katika ufundishaji baada ya dirisha la udahili kufunguliwa rasmi.
Kozi hizo zitakuwa zinafundishwa katika Kampasi zake zilizopo
Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam kwa ngazi ya Stashada, Astashahada,
Shahada za Kwanza na Shahada za Uzamili.
Sambamba na hilo Chuo hicho kimesha masomo ya Shahada za Awali
Kampasi ya Dar es Salaam, Tawi la Tegeta ambazo zitaanza rasmi mwaka wa
masomo 2020/2021.
Kozi hizo ni " Bachelor of Public Administration (BPA) na Bachelor of Accountancy and Finance- Business Sector (BAF-BS)."
Wakizungumza wakati wa usajili baadhi ya wanafunzi wamesema wameamua
kijiunga na chuo hicho kutokana na ubora wake katika ufundishaji na
kuzaliwa wanataluma wabobevu katika sekta mbalimbali.
"Huduma za Banda la Chuo Kikuu Mzumbe ni nzuri kwani wanakushauri na
kukuelekeza vizuri kuhusu kozi bora za kisoma kulingana na ufaulu wako'
alisisitiza, Amina Omary.
Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa Chuo Kikuu cha Umma kinachotoa
Elimu ya Juu nchini kikiwa na zaidi ya wanafunzi 11,000 nchi nzima.
No comments :
Post a Comment