Mwanasheri wa Dawasa, Omary Kipingu katikati akiwa na wafanyakazi wa
DAWASA, kulia ni Sofia Owe Afisa huduma wa wateja na kushoto ni Burton
Mwalupaso ambaye ni Afisa biashara DAWASA Tabata wakiwa nje ya viung vya
mahakama ya Mwanzo Ilala baada ya wadaiwa sugu hawapo pichani kumaliza
kusomewa mashtaka yao n kukiri kulipa bili zao.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WADAIWA
sugu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), wa
maeneo ya Tabata, Ubungo, na Buguruni Mnyamani wamefikishwa katika
Mahakama ya
Mwanzo Ilala kizimbani maji wa maeneo ya Tabata, Ubungo,
na Buguruni Mnyamani katika Makidaiwa bili za maji ya jumla ya Sh.
8,015,187.4.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo
na Afisa sheria kutoka DAWASA, Omary Kipingu imewataja washtakiwa
waliofika leo kuwa ni, Ahad Gurisha Mkazi wa Kisukuru, Tabata anadaiwa
2,957,162, ambapo amepunguza Sh.400,000, Tune Juma Mkazi wa Kibangu,
Ubungo anadaiwa 584,707.15,
Washtakiwa wengine ambao hawajafika
leo licha ya mahakama kutoa hati ya wito wa kuitwa mahakamani ni, David
Mgaya (Tabata) ambae anadaiwa Sh. 1,085,178.15, Rahima Sarakikya Mkazi
wa Buguruni anadaiwa 747,852.45, Hassan Khamis Mkazi wa Buguruni
Mnyamani anadaiwa Sh.733,008.45, Zacharia Okoth Mkazi wa Tabata anadaiwa
Sh.592,964.35 na Ashura Embe Mkazi wa Buguruni Mnyamani ambae anadaiwa
Sh.1,314,314.85.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya
mahakimu wawili tofauti ambapo, Gurisha na Juma wamesomewa mashtaka
mbele ya Hakimu Mkazi, Nahato na kwamb walikubali kuwa ni kweli
wanadaiwa na mamlaka hiyo.
Gurisha na Juma ,baada ya kusomewa
makosa yao na Ofisa wa Sheria kutoka Dawasa, Omary Kipingu mbele ya
Hakimu Mkazi, Nahato wa Mahakama hiyo walikubali kuwa ni kweli wanadaiwa
na mamlaka hiyo.
Hivyo, walikubali kuingia mkataba wa
makubaliano wa kulipa deni hilo hadi liishe, ambapo Gurisha amekubali
kulipa 320,000 kila tarehe 28 ya mwezi kwa miezi sita, aliahidi kumaliza
deni hilo Aprili 28, 2021.
Kwa upande wake, Juma aliyeingia
makubaliano ya kulipa dei hilo ni mama mwenye nyumba wake, Gregory
Kahwili ambae aliahidi kuwa Septemba 30,2020 atalipa 200,000, ambapo
deni lililobaki atalipa kila mwezi 100,000 litakamilika Januari 30,2021.
Hata
hivyo, Mahakama hiyo imetoa agizo la mwisho kwa wadaiwa hao kufika
mahakamani hapo, ambapo imetoa hati ya wito kwa wadaiwa hao ambao
watatakiwa kufika mahakamani hapo, Septemba 11, mwaka huu.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment