Mkuu wa Idara ya Miradi wa CAMFED, Bi. Nasikiwa Duke (kulia) akitoa mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamali kwa wasichana kutoka katika Wilaya tano za Tanzania, leo jijini Dar es Salaam. |
Na Joachim Mushi, Dar
SHIRIKA la CAMFED Tanzania limetoa
mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamali kwa wasichana kutoka
katika Wilaya tano za Tanzania, yaani Wilaya za Morogoro, Chalinze,
Handeni Mjini na Vijijini pamoja na Wilaya ya Pangani.
Akiendesha mafunzo hayo leo jijini
Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Miradi wa CAMFED, Bi. Nasikiwa Duke
amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tano na baada ya hapo kundi
hilo la wasichana wanufaika litaenda kuendesha mafunzo kama hayo ngazi
ya kata wanazotoka kwa ajili ya kueneza elimu hiyo zaidi.
Aliwataka vijana hao na wengine
nchini kujitambua wenyewe binafsi na kuwa na malengo katika maisha yao
ikiwa ni pamoja na kutambua kwamba Serikali ipo kwa ajili ya kuwawezesha
ili waweze kufikia malengo yao kupitia fursa anuai.
“…Kimsingi kila kijana akiwa na
malengo yake, nahaki ya kufika ofisi za halmashauri na kutembelea idara
ya maendeleo ya jamii na idara ya biashara akapata taarifa kamili jinsi
ya kuunda vikundi na konufaika na fursa za mikopo zinazotolewa, na
kuziangatia masharti ya mikopo hiyo,” alisisitiza Bi. Duke.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa
Maendeleo ya Ujasiriamali wa CAMFED, Sylvester Mselle akizungumza katika
mafunzo hayo, alieleza kuwa CAMFED imekuwa ikiwawezesha kundi hilo la
vijana ili kuondoka katika mnyororo wa umasikini.
Mkuu wa Idara ya Miradi wa CAMFED, Bi. Nasikiwa Duke (mbele) akitoa mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamali kwa wasichana kutoka katika Wilaya tano za Tanzania, leo jijini Dar es Salaam. |
Picha ya pamoja kati ya sehemu ya washiriki na wawezeshaji kwenye semina ya mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamali kwa wasichana kutoka katika Wilaya tano za Tanzania. |
Alibainisha kuwa wanufaika wa
mafunzo hayo ya biashara 25, wanakwenda kutoa mafunzo kwa wasichana
takribani 300 ambao watakuwa katika ngazi ya kata kwenye Wilaya
zilizotajwa, ambao nao watanufaika na mafunzo ya biashara na
ujasiriamali. Alisema mradi huo maalum unawalenga kundi la vijana
takribani 26,000 wanufaika wa CAMFED nchin zima kupitia programu ya
uwezeshaji kielimu.
Aliongeza kuwa program inayofuata
ya uwezeshaji wa wasichana wwanufaika wa CAMFED kibiashara utaongezwa na
jumla ya Wilaya 19 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania itanufaika huku
lengo likiwa ni kuwawezesha wasichana wadogo kutoka katika hali ya
utegemezi na kujitegemea kiuchumi.
No comments :
Post a Comment