Mjumbe mteule wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania Bi Irene Madeje-Mlola
Benki
ya Exim Tanzania imemteua Balozi Juma Mwapachu kuwa Mwenyekiti wake
mpya wa Bodi ya Wakurugenzi, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa
Bodi hiyo Bwana Said Mwema ambaye amemaliza muda wake kwa mafanikio
kulingana na sera ya uongozi wa benki hiyo.
Balozi
Juma V. Mwapachu ambaye kwasasa ni Mkurugenzi, Bodi ya Wakurugenzi,
kampuni ya Heritage Insurance Tanzania Limited tangu 1998, Mjumbe wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Alliance Life Assurance Tanzania Limited tangu
2014, ana uzoefu mkubwa akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali
serikalini, katika mashirika ya umma, sekta binafsi na kwenye asasi za
kiraia nchini Tanzania, kikanda na kimataifa.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari hii leo, Bodi ya Wakurugenzi ya
benki hiyo imemshukuru Balozi Mwapachu kwa uongozi wake wa mfano na
mchango wake akiwa kama Mkurugenzi katika Bodi hiyo tangu 2011
ikibainisha kuwa akiwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo Balozi Mwapachu
alihakikisha kuwa Benki hiyo inaendelea kusonga mbele kimkakati na
kiutendaji.
"Uzoefu
wake mwingi, maarifa na uongozi aliouthibitisha utazidi kuipatia benki
kasi ya kuendelea na ubunifu, kutafuta ukuaji wa baadaye, na kuimarisha
zaidi msimamo wetu tukiwa miongoni mwa taasisi kubwa za kifedha nchini,"
alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw. Jaffari Matundu wakati
akitoa maoni yake kuhusiana na uteuzi huo.
Balozi
Mwapachu ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki
(1969) Stashahada ya Juu katika Sheria za Kimataifa kutoka Chuo cha Sheria ya Kimataifa cha Indian Academy (1978),
Udaktari wa Fasihi (Honoris Causa-2005) kutoka Chuo Kikuu cha Dar-
es-Salaam na Udaktari wa Sayansi ya Siasa (honoris Causa 2012) kutoka
Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda.
Katika
uongozi wa nafasi za juu Balozi Mwapachu amewahi kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Ufaransa (2002-Aprili 2006), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (Aprili 2006-Aprili 2011) na Mwenyekiti wa Kamati ya
Watendaji Wakuu katika Utatu wa COMESA-EAC-SADC (2008-2011). Pia Balozi
Mwapachu amewahi kuwa Rais wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (SID)
kutoka 2012-2016.
Kwa
miongo kadhaa ya utumishi wake, Balozi Mwapachu ameongoza uanzishwaji
wa taasisi mbali mbali ikiwemo Chemba ya Biashara Viwanda na
Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na Baraza
la Biashara la Afrika Mashariki.
Katika hatua nyingine, Bodi ya Benki hiyo pia ilitangaza kumteua Bi Irene Madeje-Mlola kama mjumbe mpya wa Bodi.
Bi
Irene Madeje-Mlola ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara
kutoka Shule ya Masuala ya Utawala ya Maastricht ya nchini Uholanzi na
Taasisi ya ESAMI na Shahada ya Biashara (Bcom) kutoka Chuo Kikuu cha
Dalhousie nchini Canada. Bi Irene ni Mkurugenzi wa Kampuni
aliethibitishwa na Jumuiya ya Madola ya Utawala wa Kampuni na pia ana
cheti cha Uongozi wa Kimkakati wa Fedha Jumuishi kutoka Shule ya
Biashara ya Harvard. Bi Irene amebobea kwenye maeneo kadhaa ikiwemo
mabadiliko ya biashara, ujumuishaji wa kifedha, usimamizi wa miradi na
uongozi wa jumla. Kwasasa Bi Irene ni Mkurugenzi wa Uendeshaji katika
taasisi ya Financial Sector Deepening Tanzania (FSDT) akisimamia Idara
ya utaalamu na uendeshaji.
Anatarajiwa
kuongeza mchango wake wa uzoefu mkubwa kutoka katika nafasi mbali mbali
za uongozi na usimamizi alizoshikilia katika Sekta za Fedha na
Mawasiliano; baada ya kufanya kazi katika majukumu ya kimkakati na ya
uongozi katika mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Scotia, Benki
ya Royal ya Canada, Benki ya Barclays, Vodacom, Airtel, na taasisi ya
Financial Sector Deepening Tanzania (FSDT) ambayo ameisaidia katika
mabadiliko yake.
Katika
jukumu lake la sasa, Bi Irene ameshiriki katika mabadiliko makubwa na
nafasi ya ndani ambayo imefungua njia kwa shirika katika kuchochea
ujumuishaji wa kifedha na kusaidia nchi kufikia malengo ya Kitaifa.
Pamoja na uongozi wake katika ajenda ya ujumuishaji wa kifedha wa
kijinsia nchini Tanzania, alifanya kazi kwa karibu na baraza la Kitaifa
la ujumuishaji wa kifedha ili kuhakikisha wanawake na vijana wanapewa
kipaumbele katika mkakati wa Kitaifa. Irene ana uzoefu mkubwa katika
sekta ya mawasiliano na kibenki ambapo amefanya kazi katika nafasi za
uongozi wa juu ndani na nje ya nchi. Aliongoza mabadiliko makubwa katika
Sekta ya mawasiliano ambapo alisimamia utafutaji wa wafanyakazi zaidi
ya 500 kutoka nje ya shirika (outsourcing), njia iliyoongeza ufanisi
mzuri wa biashara kwa shirika.
“Akiwa
hodari katika ukuzaji wa mifumo mpya, usimamizi mzuri na uanzishaji wa
shughuli ndogo ndogo katika mashirika, Irene anabeba haiba ya uvumbuzi
na fikra za kimkakati ambazo zitakuwa muhimu kwa ukuaji wa Benki yetu”
alisema Matundu.
No comments :
Post a Comment