Balozi wa China nchini Mhe.
Wang Ke akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
wakati walipokutana kwa majadiliano leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Brigedia Jenerali
Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
************************************
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali
Wilbert Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini
Mhe. Wang Ke pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni
katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Balozi Ibuge
amesema kuwa pamoja na mambo mengine, waliweza kujadili umuhimu wa
kuongeza ushirikiano hussusan katika sekta ya biashara na uwekezaji
pamoja na utalii.
“Tumezungumzia kuhusiana na
miradi mbalimbali ambayo tumekuwa tukishirikiana na China katika kukuza
maendeleo endelevu,” amesepa Balozi Ibuge
Balozi Ibuge ameongeza kuwa
Tanzania na China zitaendelea kuimarisha mashirikiano katika sekta za
kilimo na utalii kwa sababu ni sekta ambazo zikiimarishwa vizuri zaidi
zitakuza uchumi haraka zaidi.
Nae Balozi wa China, Mhe. Wang
Ke amesema kuwa Serikali ya China imejidhatiti kuimarisha uhusiano wake
na Tanzania hasa baada ya janga la COVID 19 ili kuhakikisha kuwa nchi
hizi mbili zinakuwa na uchumi imara.
Katika tukio jingine, Katibu
Mkuu Balozi Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia
nchini, Mhe. Roberto Mengoni ambapo wamejadiliana mambo mengi
yanaohusiana na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na
China.
“Italia na Tanzania ni
marafiki wa muda mrefu katika mazungumzo yetu tumejadili namna ya
kuimarisha mashirikano na namna ya kuendeleza na kuboresha sekta za
biashara na uwekezaji, elimu na utalii,” amesema Balozi Ibuge.
Kwa upande wake Balozi Mengoni
amesema kuwa wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano na
kukubaliana kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kukuza uchumi wa
mataifa yetu.
Viongozi hao wamejadiliana na
kubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya
mataifa hayo mawili ambao umejikita katika sekta za elimu, utalii
pamoja na biashara na uwekezaji.
No comments :
Post a Comment