Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizindua moja
la jengo la watumishi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akitoa maelezo kwa fundi anayejenga madarasa yaChuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa madarasa katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Madarasa yenye ukumbi wa Mikutano katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizungumza na watumishi pamoja na wanafunzi wa chuo cha Hombolo wakati wa uzinduzi wa madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo., Dk.Mpamila Madale,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa program ya kutoa shahada ya utawala na menejimenti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Hombolo mara baada ya kuzindua madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma
Baadhi ya wanafunzi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,wakati wa kuzindua program ya kutoa shahada ya utawala na menejimenti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Hombolo pamoja na madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,akigawa vyeti kwa wana kikundi cha ngoma mara baada ya kuzindua program ya kutoa shahada ya utawala na menejimenti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Hombolo pamoja na madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma
Sehemu ya watuishi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,wakati wa kuzindua program ya kutoa shahada ya utawala na menejimenti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Hombolo pamoja na madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua program ya kutoa shahada ya utawala na
menejimenti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Hombolo pamoja na madarasa na nyumba za walimu wa chuo hicho kilichopo nje ya jiji la Dodoma………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameupongeza uongozi wa chuo cha Serikali za
Mitaa (LGTI) kwa kutumia Zaidi ya Sh.Milioni 747 zilizotokana na mapato
ya ndani ya chuo hicho kuboresha miundombinu ya elimu chuoni hapo na
kuongeza mvuto na hamasa kwa wasomi wa kada hiyo nchini.
Mhe.Jafo amebainisha hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi
katika uboreshaji huo na kuzindua kwa program ya kutoa shahada ya
utawala na menejimenti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, uliofanyika
katika ukumbi wa Mikutano, Hombolo Jijini Dodoma.
Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa uongozi wa chuo cha Serikali za
Mitaa (LGTI) kwa kutumia mapato ya ndani kujenga kuboresha miundombinu
ambayo ni kumbi za miadhara, madarasa na nyumba za waalimu.
“ hatua hiyo ni ya kuigwa kwani ni chuo cha kwanza kilichoweza
kupiga hatua ya kujenga majengo kwa kutumia mapato ya ndani jambo ambalo
ni lamkipekee nchini”, ameeleza Mhe. Jafo.
Ujezi wa jengo la kwanza la miadhara lenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 500 limegharimu Shilingi milioni 246, ukumbi wa pili
umegharimu Shilingi 226, madarasa mawili ambayo kila mmoja linauwezo wa
kuchukua wanafunzi 250 linagharimu shilingi milioni 274 na nyumba yenye
thamani ya milioni 99,majengo haya yote yamejengwa kwa kutumia “Force
Account”
Mhe.Jafo ametoa wito kwa vyuo vyote vya Serikali kuiga mfumo wa
Chuo cha Serikali za Mitaa ambao wametumia mapato yao ya ndani kuongeza
majengo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kuwa katika mazingira mazuri
ya kujifunza na kufundishia.
Waziri Jafo amepongeza hatua ya uongozi wa chuo hicho kwa
kutekeleza agizo la kuanza kutoa shahada ya kwanza na kusisitiza haja ya
chuo hicho kuangalia namna ya kuanza na shahada ya ukutubi ili
kuwarahisishia wananchi wanaotaka kujiendeleza au kusoma fani hiyo.
Naye, Mkuu wa Chuo hicho
Dkt.Mpamila Madale amesema kuwa uwepo wa ongezeko la wanafunzi
limechangia kuongeza mapato ya ndani ambayo yamefanya kuboresha
miundombinu ili ikidhi mahitaji ya ongezeko hilo.
Ameeleza kuwa chuo kina mkakati wa kujenga jengo la
utawala,ujenzi wa jengo katika tawi la miji ili kuondokana na adha ya
kulipa pango inayowakumba kwa sasa ambapo wamekuwa wakilipa Shilingi
milioni 75 kwa mwaka
Madale ameongeza kuwa kwa sasa wako katika hatua za kuandaa
mitaala kwa ajili ya kuanzisha kozi za shahada ya utawala na rasilimali
watu, shahada ya ukutubi na Maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake Meneja wa Milki, Mhandisi Frank Massawe amesema
katika awamu ya kwanza wameweza kujenga jengo moja lenye nyumba mbili za
watumishi ambapo mpango wa chuo ni kujenga majengo 10 kwa kutumia
mapato ya ndani.
No comments :
Post a Comment