Friday, August 14, 2020

RAIS MAGUFULI ATUNUKIWA TUZO NA BARAZA KUU LA TAG


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo ametunukiwa tuzo ya ufanisi katika kuliongoza taifa pamoja na kulishinda janga la Corona (COVID-19) hapa nchini ambapo Mgonjwa wa kwanza kupatikana hapa nchini alitangazwa Machi 16,2020.

Tuzo hiyo ametunikiwa na Kanisa la Tanzania Asemblis of God (TAG) leo wakati akizungumza na Baraza kuu la kanisa hilo katika ukumbi wa chuo cha biblia Mijuji jijini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli akipokea Tuzo kutoka kwa Baraza Kuu la TAG.

 

No comments :

Post a Comment