Friday, August 14, 2020

EMIRATES YAZIDI KUCHANJA MBUGA KIMATAIFA


SHIRIKA La ndege la Emirates tayari limepeleka ndege yake ya A380 katika

mjini Guangzhou tangu Agosti 8 mwaka huu, pia Emirates imeanzisha safari za Amsterdam na Cairo kupitia ndege ya A380 na hiyo ni pamoja na safari za London Heathrow na hiyo ikiwa ni katika kushughulikia masoko na kuwapa wateja machaguo zaidi ya kusafiri.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeeleza kuwa Emirates imerejesha huduma ya A380 kwa miji mitano na itaendelea kupanua zaidi wigo wa huduma za anga.

Imeelezwa kuwa kupitia Emirates A380 wateja wataweza kufurahia huduma za kila siku za Amsterdam, safari za Cairo mara nne kwa wiki, safari za London Heathrow mara mbili kwa siku, Paris mara moja kwa siku na mara moja kwa wiki kwa safari za Guangzhou.

Imeelezwa kuwa hadi sasa Emirates imerejesha safari kutoka Dubai kwenda Addis Ababa, Cairo, Dar es Salaam, Nairobi, Prague, Sao Paulo, Stockholm na Seychelles na hiyo ni pamoja na kuimarisha huduma za usalama ambapo hadi sasa miji 68 imerejeshewa huduma na kuweza kufikia asilimia 50 ya utoaji huduma za anga mara baada ya janga la Corona.

Aidha imeelezwa kuwa kwa abiria kutoka Amerika, Ulaya, Afrika, Mashariki ya kati na Asia sasa wanaweza kufurahia safari zao kupitia Dubai kwa kuwa jiji hilo tayari limefunguliwa kwa biashara za kimataifa na mapumziko.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa vipimo vya Covid-19 ni lazima kwa abiria wote wa ndani na wanaowasili Dubai na UAE na raia wake pamoja na watalii bila kujali nchi wanazotoka.


Mwisho.

 

No comments :

Post a Comment