NI wazi kuwa mapinduzi ya kidigitali yamekuwa na mabadiliko makubwa katika namna watu wanavyoishi kwenye miaka ya karibuni.
Kwa bahati nzuri, mabadiliko haya yamekuja na fursa mbalimbali na pia yameipatia Tanzania nafasi ya kukuza uchumi wake Zaidi.
Katika
ripoti yake ya hivi karibuni Benki ya Dunia iliainisha kuwa mapinduzi
ya teknolojia ya kidigitali yataweza kupelekea mabadiliko zaidi juu ya
namna watu wanavyofanya kazi duniani kote katika nyanja mbalimbali.
Uchambuzi
wao ulibainisha kuwa ufumbuzi wa kidigitali umesaidia kuchocheza
ubunifu ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha kwenye simu na ufanyaji
biashara kidigitali.
Ifahamike
kuwa kwa miaka kadhaa sasa, mapinduzi ya kidigitali yamekuwa jambo
kubwa nchini Tanzania na katika miji kama Dar es Salaam imeona
teknolojia ukikua zaidi na zaidi kila leo.
Ukuaji
katika eneo hilo kwa kiasi fulani kumechangiwa na jitihada zilizofanya
na makampuni za mawasiliano nchini Tanzania kuwekeza katika sekta
mbalimbali zinazokua. Kwa ujumla, uwekezaji huu umekuwa na matokeo
chanya kwa wananchi, wafanyakazi na wafanyabiashara.
Kwa
mfano, Huduma ya fedha kwenye simu ya Tigo Tanzania (Tigo Pesa)
imezisaidia biashara kuwa na njia imara na ya haraka kuweka fedha, kutoa
na kutuma fedha. Bila kuwa na ulazima wa kufika kwenye tawi la benki
wafanyabiashara wanaweza kufuatilia miamala yao na kufanya malipo kwa
wasambazaji bidhaa kwa urahisi zaidi.
Aidha,
huduma ya Tigo Business ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwasaidia
wafanyabiashara wadogo na wa kati, imekuwa msaada mkubwa kwa biashara na
wafanyakazi wake kufkia fursa za kibiashara. Kwa mfano, upatikanaji wa
intaneti ya uhakika kwenye simu umekuwa na mchango mkubwa kusaidia
biashara kutangaza biashara zao na huduma, pamoja na kuwasiliana na
wateja wake.
Licha
ya faida hizo kufurahiwa na wateja wa Tigo kwa muda sasa, wengi
wanaamini kuwa huduma hizo zitaanza kufurahiwa na wateja wa Zantel.
Mwishoni mwa mwaka jana watoa huduma hao (Tigo na Zantel) walitangaza
kusudio la kuungana. Mara muunganiko huo utakapokamilika wateja kutoka
makampuni hayo wataweza kufurahia huduma zinazotolewa na kampuni zote
mbili.
Hii
ina maana wateja wa Zantel wataweza kutumia huduma kama Tigo Pesa na
Tigo Business. Matarajio ya watumiaji wengi wa simu ni kuwa mchakato
mzima wa kuungana kwa kampuni hizo utakamilika mapema ili wateja waweze
kufurahia faida zake.
No comments :
Post a Comment