Mkurugenzi
wa Selcom Tanzania Sameer Hirji akimjazia mafuta moja ya washindi wa
kampeni ya Achana na Cash, lipa kidijitali tukupige Full tenki iliyokuwa
inaendeshwa na Kampuni ya Selcom pamoja na Puma Energy, Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhalla
Mmoja
ya washindi wa Kampeni ya Achana na Cash, lipa kidijitali tukupige Full
tenki, Paulo John akiwashukuru kampuni ya Selcom kwa kuanzisha kampeni
hiyo na kuwaasa watanzania kutumia mfumo wa kidijitali kwenye malipo
kwani una faida kubwa sana na inaepusha msongamo.
Moja ya washindi akihakikisha gari yake inajaa mafuta
Mkurugenzi
Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhalla akimjazia mafuta moja
ya washindi wa kampeni ya Achana na Cash, lipa kidijitali tukupige Full
tenki iliyokuwa inaendeshwa na Kampuni ya Selcom pamoja na Puma Energy,
Kulia ni Mkurugenzi wa Selcom Tanzania Sameer Hirji.
KAMPUNI
zalendo za Selcom na Puma Energy, leo tarehe 13 Agosti zimeendelea
kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania kurasimisha malipo hasa
katika sekta ya nishati. Kampuni hizo zimefanya hivyo kwa kuendeleza
kampeni yao ya “Achana na cash, lipa kidijitali tukupige full tenki” kwa
muda wa wiki mbili za ziada mpaka 31 Agosti 2020.
Kampeni
hiyo ilianza tarehe 4 Juni na kupangwa kuisha tarehe 4 Agosti 2020.
Aidha kutokana na muamko mkubwa wa wateja, kampuni hizo zimeamua
kuendeleza kampeni hiyo ili kuwapa Watanzania wengine 10 fursa ya
kuzawadiwa full kwa kulipa kidijitali katika vituo vya Puma Energy.
Hayo
yamebainika katika halfa fupi ya kuwazawadia full tenki washindi 10 wa
awamu ya kwanza iliyofanyika katika kituo cha Puma Energy Upanga.
Akigongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Selcom,
Baguma Mpenda amesema kwamba dhamira kuu ya kampeni hiyo ni kuhimiza
Watanzania kuendelea kufanya malipo kidijitali kupitia SelcomPay
Mastercard QR kwani ni rahisi na salama zaidi na si kuwashindanisha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic
Dhalla alisema “Puma ni kinara wa malipo ya kidijitali nchini
ukilinganisha na makampuni mengine ya nishati ya mafuta. Tuna njia zaidi
ya moja za malipo ya kidijitali zikiwema SelcomPay Mastercard QR na
Puma Elite Card ambazo zinatumika katika vituo vyetu vyote nchini.”
Dhamira
ya kampuni hizi kurasimisha malipo ni dhahiri kwani siyo mara yao ya
kwanza kuendesha kampeni kama hii kuhimiza malipo ya kidijtali. Mnamo
Novemba 2019 ziliendesha kampeni ya Bomba Weekends ambayo iliwapa wateja
waliolipa kidijitali kupitia SelcomPay Mastercard QR rejesho la 5%.
“Tumeona
ongezeko kubwa la malipo ya kidijitali ndani ya miaka michache
iliyopita. Kikubwa na muhimu ni kwamba Watanzania wanaendelea kuibeba
dhamira ya serikali ya kurasimisha uchumi wa nchi yetu kwa kufanya
malipo kidijitali. Tumeona hili si kwa Puma na sekta ya nishati tu, bali
pia katika sekta zingine tunazojihusisha nazo. Kazi yetu kama Selcom ni
kuboresha na kurahisisha teknolojia hii ya malipo hadi kumfikia kila
Mtanzania. Tunataka kufika wakati hadi machinga waweze kupokea malipo na
kufanya matumizi wakihitaji kupitia SelcomPay/Mastercard QR.” Alisema
Mkurugenzi wa Selcom, Sameer Hirji.
Akiongea
katika hafla hiyo, mmoja wa wazawadiwa hao Washngton Onyango alisema
anavutiwa kutumia huduma ya SelcomPay/Mastercard QR kwa sababu ni
rahisi, salama na haina makato yoyote kwa mteja kama ada ya kukamilisha
muamala. “Unalipa kama ilivyo na uzuri ni kwamba inapokea malipo kutoka
mitandao yote ya simu na baadhi ya mabenki.” Aliongeza Onyango.
No comments :
Post a Comment