Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiipongeza UNDP kwa msaada waliotoa
kutengeneza magari yatakayotumika kubeba watalii pindi watakapopatwa na
dharura za maradhi, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo
iliyofanyika kwenye ofisi za Hanspaul, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akikata utepe pamoja na Muwakilishi
Mkazi wa UNDP Tanzania Bi. Christine Musisi pamoja na viongozi wengine,
wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari ya dharura (ambulance)
iliyofanyika katika ofisi za Hanspaul, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa ndani ya gari la dharura
(ambulence) mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo
yatakayo hudumia watalii, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa ameambatana na Muwakilishi Mkazi
wa UNDP Tanzania Bi. Christine Musisi (katikati) pamoja na moja ya
wakurugenzi wa kampuni ya Hanspaul, Bw. Satbir Singh Hanspaul wakati wa
hafla fupi ya Makabidhiano wa magari manne ya dharura yaliyotolewa na
Chama cha Makala wa Utalii Tanzania (TATO), Jijini Arusha.
……………………………………………………….
Katika kipindi ambacho Ugonjwa wa
Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya
Corona (COVID-19)
uliikabili ulimwengu, sekta binafsi kwa kushirikiana na sekta ya Umma
ilifanya kazi kwa pamoja kutengeneza mkakati wa uendeshaji wa shughuli
na biashara ya utalii katika kipindi hicho.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Arusha
na Katibu Mkuu Wizara ya Malisiali na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki
wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika
Warsha ya kupokea maoni ya wadau wa utalii katika kuandaa mkakati wa
kurejesha sekta ya utalii katika hali yake ya awali baada ya mapambano
dhidi ya COVID-19.
‘’Tulitengeneza Mkakati huo ambao
unaitwa Standard Oparate Procedures ili kuhakikisha kwamba tunaishi na
ugonjwa huu kwa maana ya kwamba tusisimamishe shughuli za kuwapokea
watalii lakini tujue namna ya kuwapokea watalii ili kusudi watalii wawe
salama na watoa huduma wawe salama’’ amesema
Katika Mkakati huo amesema
waliahidi kwamba katika maeneo yao ya utalii wataweka magari ya kubebea
wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuandaa maeneo ambayo yatasaidia kutoa
huduma pale ambapo ikitokea watalii wamepata tatizo ama watoa huduma
wamepata tatizo waweze kuhudumiwa katika vituo vya kutolea huduma za
Afya.
Wakati huo huo amelishukuru
Shirika la UNDP kwa kushiriki kuandaa na kuboresha magari ya kubebea
wagonjwa kwa kuyabadilisha magari hayo kutoka magari ya kawaida na kuwa
magari ya kubebea wagonjwa ambayo yatasaidia kuhudumia watalii
watakaopata dharura za maradhi pindi wakiwa katika ziara zao.
‘’Tunalishukuru Shirika la hili la
UNDP limefadhili pamoja na kugharamia magari hayo. Tunashukuru sana kwa
kutusaidia na sasa wanatusaidia kazi nyingine maarufu na muhimu sana
ambayo ni ya kutengeneza mkakati wa kurejesha hali ya utalii kama ilivyo
kuwa awali’’
No comments :
Post a Comment