Mkulima wa zabibu Daniel Ngoima wa Kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma akivuna zao hilo kama alivyokutwa shambani kwake
Mkulima wa zabibu Victoria Zablon wa kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma akionja sukari ya zao hilo
Baadhi ya wakulima wa zao la
zabibu Kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma wakiwa na makreti
yenye zao hilo baada ya kuvuna tayari kwa kusafirishwa kupelekwa
kiwandani kwa ajili ya uzalishaji wa vinywaji
…………………………………………..
Kampuni ya
Tanzania Distilleries Limited (TDL), imeeleza dhamira yake ya kuendeleza
kilimo cha zabibu mkoani Dodoma pamoja na matarajio yake ya kuingia
mikataba ya
kununua zabibu moja kwa moja kutoka kwa wakulima wadogo.
Mchango wa TDL
wa sera yake ya kununua malighafi nchini na dhamira ya kukuza sekta ya
kilimo cha zabibu inaenda sambamba na jitihada za serikali za
kuboresha maisha ya wakulima wadogo na kukuza uchumi wa Tanzania.
TDL inaamini
jitihada za Serikali za kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda zinaweza
kufanikiwa ikiwa wakulima wadogo wanawezeshwa kuzalisha malighafi
inayohitajiwa na viwanda.
Meneja Mkuu wa
TDL, Devis Deogratius, alisema kampuni hiyo kwa sasa inanunua takribani
lita milioni 1.2 za mchuzi wa zabibu kwa mwaka kutoka kampuni za
CETAWICO na UWAZAMAM, ambazo zinanunua zabibu za wakulima wa ndani
ambapo inatumia bilioni 3.3 kwa mwaka.
Deogratius
aliongeza kusema kuwa imedhamiria kununua malighafi ya ndani katika
kipindi chote cha miaka ijayo ambapo kwa sasa inatumia malighafi na
huduma za kufanikisha uzalishaji kwa asilimia 80% ambayo ni sasa na
shilingi bilioni 46.
TDL imewekeza
katika uundaji wa chapa za Kitanzania ambazo ni pamoja na: Imagi,
Valeur, Wines Dodoma, Dodoma Rose, Konyagi na Zanzi Cream liqueur ambazo
zimetengenezwa kwa viwango vya ubora kwa kimataifa kwa kulenga
mahitaji ya makundi mbalimbali katika soko.
No comments :
Post a Comment