Monday, August 3, 2020

WAZIRI JAFO:UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA MSINGI NI CHACHU YA KUIMARISHA UCHUMI WA KATI



 WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo akifanya mazoezi ya kukimbia na watumishi wa TAMISEMI kabla ya kuwasilsha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya  Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye  ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’  iliyofanyika Jijini Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo akivishwa medali na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Maswala ya Afya TAMISEMI , Dkt. Dorothy Gwajima kama ishara ya kumpngeza kwa mafanikio ya miaka miaka mitano katika sekta ya Afya TAMISEMI leo katika viwanja vya Michezo Shule ya Sekondari Dodoma 
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo wakati akitoa zawadi kwa mama aliyejifungua leo katika kituo cha afya cha Makole Jijini Dodoma
Baadhi ya watendaji kutoka mamlaka za Serikali za Mitaa katika  sekta ya Afya wa kimfatila WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo wakati akiwa katika picha na mama aliyejifungua leo katika kituo cha afya cha Makole Jijini Dodoma
 WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo wakati (kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole alipofika kuwaona wakina mama waliojifungua leo kabla ya kutoa  mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya  Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye  ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’  iliyofanyika Jijini Dodoma 
Baadhi ya watendaji kutoka mamlaka za Serikali za Mitaa katika  sekta ya Afya wa kimfatila WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya  Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye  ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’  iliyofanyika Jijini Dodoma
………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
Serikali  imesema  uboreshaji wa Huduma ya Afya  Msingi ni nguzo muhimu katika
kuimarisha uchumi wa kati kwani uimara wa afya za watanzania ndo chachu ya kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo  na WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani  Jafo wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya  Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye  ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’  iliyofanyika Jijini Dodoma.
Aidha katika hafla hiyo Waziri  Jafo  amejikuta akibubujikwa  na machozi namna wananchi walivyo kuwa wakipata adha na kupoteza maisha kutoka na ukosefu wa huduma za afya kwenye baadhi ya maeneo nchini jambo lililokuwa linadhohofisha afya za wananchi katika utafutaji wao kutokana na kutokuwa na afya imara.
 Waziri Jafo amesema kwa wananchi wengi wa likuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za afya, lakini kwa kipindi cha miaka mitano ya serikali chini ya Rais John Magufuli imetoa kipaumbele kwa sekta hiyo na kuondoa adha kwa wananchi  hivyo kuchagiza katika utafutaji wa kipato .
“Kuna  watu wenye uwezo hawa fahamu kwamba watanzania walikuwa wanateseka,  walikosa kupata huduma bora za afya, na wanasafiri zaidi ya kilometa  140  kufua tahuduma za afya, kina mama wanapata matatizo ya fistula, baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na vituo vipo mbali,” ameeleza Waziri Jafo.
Waziri Jafo ameongezea kuwa Watu hawafahamu kuna wakina mama wangapi wamekufa kwa kukosa huduma muhimu wengine wamesafirishwa kwa baiskeli na mikokoteni kufata huduma za afaya.
Waziri Jafo ameweka wazi kuwa watanzania wanaoishi mijini hawafahamu kama Taifa limepoteza watu wengi kwa kukosa huduma.
“Leo Rais Magufuli  amekuja na maono mapana ya kuhakikisha anaokoa maisha ya watanzania kwa kuwasogezea hudumaza afya  karibu na kutaka watendaji wa huduma za afya kutekeleza weledi wao  kwa ufasaha kwa kutoa huduma bora kwa watanzania wote nchini bila upendeleo.
Aidha, Waziri Jafo amesema nchi tangu ilipopata uhuru hadi Rais Magufuli anaingia madarakani kulikuwa  na  Hospitali za wilaya 77 katiyaHalmashauri 185.
“Mpaka sasa kwa awamu ya kwanza hospitali 67 zimekamilika, zikaongezwa zingine na sasa jumla ya hospitali   99 zinajengwa, hizo za kwanza zimeanza kutoa huduma na hizo zingine zipo hatua mbalimbali ya ujenzi, tuna kila sababu ya kumshukuru Rais,”ameeleza Waziri Jafo.
Pia Waziri Jafo amesema zaidi ya zahanati 1198 zimejengwa kwa kipindi cha miaka mitano.
“Niwashukuru wataalam wangu, kwa kuwa wamekuwa ni injini ya kuhakikisha  mambo yanasonga katika sekta ya afya, idara hii ilikuwa mfu lakini Rais ameibeba idara hii  na  sasa inafanyakazi katika ubora unaohitajika na watanzania,”ameshukuru Waziri Jafo.
Waziri Jafo amebainisha kuwa wakinamama wajawazito waliojifungua katika vituo hivyo vipya ni  219,764  na waliopata huduma ya upasuaji ni 18,826.
Huku Wagonjwa wengine wakiwemo kina baba zaidiya 6,000 wamefanyiwa upasuaji wa kawaida kwenye vituo hivyo, na kina baba wengine wametengeneza familia zao katika vituo hivyo,  wazee zaidi ya 100,000 wamepata huduma,”ameweka bayana  Waziri Jafo.
Lakini pia katika hatua nyingine  Waziri Jafo ametembelea kitu cha afya cha Makole na Kutoa zawadi ya sabuni, maziwa na maji kwa wakina mama waliojifungua kwa siku ya leo akiwambia leo ni siku ya Afya TAMISEMI ikionyesha mafanikio yaliyofanyika ndani ya miaka mitano katika sekta ya afya hapa nchini.
Awali, Mwakilishiwa Katibu Mkuu Wizara  ya Afya,  Maendelo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Grace Maghembe, amesema kuwa kuna mikoa mitano ili kuwa haina kabisa hospitali  za rufaa za mikoa, lakini kwa sasa zimejengwa na zinatoa huduma katika ubora wa hali ya juu.
“Uboreshaji wa huduma za afya ikiwemo za kibingwa nchini umechangia kupunguza idadi ya wagonjwa wa kupelekwa nje ya nchi”, aesema Maghembe.
Kwa upande wake  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk.Dorothy Gwajima amesema kuwa uwepo wa miundombinu hiyo inatakiwa kwenda  sambamba   na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili kuwa vutia watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF).

No comments :

Post a Comment