Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akizungumza kwenye siku
maalum ya kuhamasisha ushirika kwenye maonesho ya Nanenane Nyakabindi
leo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki
akiongea wakati alipohutubia kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu
ikiwa ni siku maalum ya kuhamasisha ushirika wakati wa maonesho ya
Nanenane akimwakilisha Waziri Mkuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Angellah Kairuki akikabidhi mfano
wa hundi ya shilingi milioni mbili na nusu kwa kiongozi wa chama cha
ushirika CHAURU kwa ajili ya kuhamasisha ushirika.
Picha ya viongozi meza kuu kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bw.Gerald Kusaya, Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga ( katikati)
na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu ) Uwekezaji) Mhe.Angellah
Kairuki wakifuatilia matukio wakati wa siku maalum ya ushirika kwenye
viwanja vya Nyakabindi Simiyu leo.Waziri
wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga akizungumza wakati wa maonesho ya kilimo
Nanenane leo kuhusu kuhamasisha ushirika katika viwanja vya Nyakabindi
mkoani Simiyu.
Picha na habari na Wizara ya Kilimo.
**********************************
Wizara ya Kilimo imepongezwa kwa
uamuzi wa kuvifuta vyama vya ushirika 2,539 ambavyo vilikuwa na utendaji
mbovu uliosababisha kero kwa wanaushirika nchini.
Pongezi hizo zimetolewa leo
(03.08.2020) na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji )
Angellah Kairuki wakati alipohutubia wananchi wa
Simiyu kwenye maonesho
ya Nanenane ikiwa ni siku maalum ya kuhamasisha ushirika.
Amesema hatua hiyo ya wizara
itawezesha wanaushirika ambapo ni wakulima, wavuvi na wafugaji kunufaika
na kazi zao ndani ya ushirika .
“ Ninawapongeza sana Wizara
kwa hatua mliyochukua ya kuvifuta vyama vya ushirika 2,539 kwa sababu ya
kutofanya kazi iliyokusudiwa.” alisema Waziri Kairuki.
Waziri Kairuki alisema katika
kipindi cha 2018/2019 jumla ya viwanda 75 vimeanzishwa na vyama vya
ushirika vinavyochata alizeti, chikichi,kutengeneza samani za
majumbani,kuchakata pamba na mazao ya nafaka pamoja na usindikaji wa
maziwa.
“ Viwanda vinavyomilikiwa na
vyama vya ushirika vimeongezeka kutoka viwanda 133 mwaka 2018 hadi
kufikia viwanda 208 mwaka 2019” alisema Waziri Kairuki.
Katika hatua nyingine Waziri
Kairuki ameiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika kushirikiana na Wakala
wa Serikali Mtandao (EGA) kuangalia namna bora ya kuweka mfumo
shirikishi wa TEHAMA utakaoweza kuongeza uwazi katika usimamizi wa vyama
vya ushirika hususan AMCOS.
Naye Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga amesema wizara yake itaendelea kuhakikisha wakulima, wavuvi na
wafugaji nchini wananjiunga na vyama vya ushirika ambavyo vitawasaidia
kupata nguvu ya kuweza kupata mitaji,masoko,pembejeo na huduma za ugani
ili wakuze uzalishaji.
Maonesho ya Kilimo ya Nanenane
Kitaifa yameingia siku ya tatu leo ambapo wananchi na wakulima toka
mikoa ya Mara,Simiyu na Shinyanga wanaendelea kupata elimu kwenye
mabanda na vipando vilivyoandaliwa.
Kauli mbiu ya Nanenane mwaka huu inasema “ Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”
No comments :
Post a Comment