Katibu
mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (sera, uratibu na uwekezaji), Dorothy
Mwaluko, Dorothy Mwaluko (kulia) akikabidhi mkataba wa makubaliano ya
utekelezaji wa programu maalumu ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara
mkoani Geita (MOU) kwa Makamu wa Rais wa kampuni ya GGML, Simon Shayo
(kushoto).
Mkurugenzi
wa Baraza la Uwezeshaji Watanzania kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa
(kushoto) na Mwanasheria mwandamizi wa GGML, David Nzaligo GGML (kulia),
wakisaini mkataba wa kuwajengea uwezo watanzania kupata zabuni kwenye
sekta ya migodi. GGML imedhamini mafunzo hayo.
Makamu
wa Rais wa kampuni ya GGML, Simon Shayo (kushoto) akizungumza baada ya
kusaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa programu maalumu ya
kuwajengea uwezo wafanyabiashara mkoani Geita (MOU).
NA MWANDISHI WETU
Kampuni
ya Uchimbaji wa Madini ya Geita (GGML) kwa kushirikiana na Baraza la
Kitaifa la Uchumi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), imesaini
makubaliano ya utekelezaji wa programu maalumu ya kuwajengea uwezo
wafanyabiashara mkoani Geita kushiriki kikamilifu katika zabuni
zinazotolewa na mgodi huo.
Makubaliano
hayo yaliyotiwa saini Julai 20, mwaka huu mkoani Geita, yatadumu kwa
kipindi cha mwaka mmoja hadi Juni 30, mwaka 2021.
Akizungumza
katika hafla ya kusaini makubaliano hayo na kuzindua program hiyo,
Makamu Rais wa GGML, Simon Shayo alisema progamu hiyo pia inalenga
kuwajengea uwezo wazabuni wa Mkoa wa Geita ili kuweza kutambua na
kuzingatia viwango na ubora wa bidhaa na huduma zinazohitajika katika
shughuli za GGML.
Aliongeza
kuwa program hiyo, pia inalenga kuwaunganisha wazabuni wa GGML na
mamlaka mbalimbali za Serikali, sekta binafsi na jamii kwa ujumla
zinazotoa fursa zinazowezesha kushiriki kikamilifu katika zabuni hizo.
“Programu
hii itawawezesha wazabuni wa GGML kupata soko la uhakika la bidhaa na
huduma wanazozalisha hivyo kujiongezea kipato cha mtu mmoja mmoja,
kipato cha kaya na jamii kwa ujumla hivyo kuchangia pato la Taifa kwa
upande mmoja,” alisema.
Aidha,
alisema GGML itaweza kupata huduma na bidhaa zenye ubora kutoka kwa
wazabuni wa ndani zitakazoongeza tija kwa wazalishaji wa ndani.
"GGML
tumejitolea katika maendeleo endelevu ya jamii inayotuzunguka. Tunapenda
kuacha urithi, hata wakati madini yatakapokuwa yameisha kuchimbwa.
Kusudi letu ni kuongeza ushiriki wa watanzania kwenye shughuli za mgodi
ili tuweze kusaidia jamii ambayo tunafanya nayo kazi. Tumekuwa
tukionyesha haya huko Geita kwa kuwa washirika dhabiti na Serikali
katika kuboresha huduma za kijamii, elimu, afya na kilimo, "alisema
Simon Shayo
Shayo
alifafanua kuwa, GGML inajivunia kuwa walipa kodi bora na wakubwa nchini
Tanzania ambapo mwaka 2019 pekee, jumla ya kodi iliyolipwa na GGML kwa
serikali ya Tanzania ilikuwa takriban Sh bilioni 467 sambamba na kutoa
ajira kwa watanzania zaidi ya 5000.
Akizungumza
katika uzinduzi wa program hiyo, Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(sera, uratibu na uwekezaji), Dorothy Mwaluko alisema programu hiyo
imetengenezwa wakati muafaka.
“Itahakikisha
changamoto ambazo zinafanya kampuni za kitanzania kushindwa kupata
zabuni kwenye uwekezaji unaofanyika nchini, zinatatuliwa na kumwezesha
mwekezaji kutekeleza kikamilifu sheria za nchi kwa kununua bidhaa na
kutumia huduma za watanzania zinazokidhi viwango.
“Nipende
kuwapongeza Kampuni ya Uchimbaji wa Geita, GGML kwa kukubali kuwezesha
programu hii kwa kuwa wafanyabiashara watakaonufaika na mafunzo haya
mbali na kushiriki shughuli za uzalishaji katika mgodi huu, pia
yatawafungulia njia kushiriki katika miradi inayotekelezwa kwenye sekta
zingine,” alisema.
Aidha,
Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa alisema uzinduzi wa programu hii
unabebwa na kauli mbiu isemayo ‘‘Ushiriki na Ushindani wa Uwazi katika
Kukuza Uchumi’’.
Alisema
kauli mbiu hiyo inajielekeza katika kujenga uwezo kwa wafanyabiashara
wa ndani ili wapate fursa ya kushiriki katika sekta ya madini.
No comments :
Post a Comment