Baadhi
ya wananchi wa Kigamboni, wameipongeza Serikali na Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutokana na kuusimamia vizuri mradi wa ujenzi wa
barabara inayounganisha Daraja la Nyerere ambayo ipo kwenye hatua za
mwisho kukamilika.
Walitoa pongezi hizo na
kuonesha hisia zao mwishoni mwa wiki mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista
Mhagama wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wenzake, Meja Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Adiel Raphael Kaaya, alisema mradi huo ni miongoni mwa
miradi ambayo inaonekana dhahiri na kama kuna mtu ambaye ni mmbishi
aende akashuhudie ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni nzuri na yenye ubora
wa hali ya juu.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
William Erio, aliishukuru Rais Dkt. Magufuli kwa sababu yanayofanyika ni
matokeo ya maelekezo yake baada ya mkwamo wa muda mrefu wa kipande
hicho cha barabara.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akishuhudia mafundi wakiendelea na kazi
ya usambazaji wa lami katika barabara inayounganisha Daraja la Nyerere,
Kigamboni, mwishoni mwa wiki.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni.Mwendesha Bodaboda, Godfrey Kurumwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, ambapo aliipongeza Serikali kwa kukamilisha mradi huo wa barabara.
No comments :
Post a Comment