TAKUKURU
inamshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya White Star
Investment Taalib Karim Mbowe, inayofanya biashara ya usafirishaji ndani
na nje ya nchi kwa makosa ya ukwepaji wa kodi, udanganyifu na
utakatishaji wa fedha haramu.
Taarifa
hiyo imetolewa leo Agosti 16, 2020, na Afisa Uhusiano wa TAKUKURU
Doreen Kapwani, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia
Jenerali John Mbungo, ambapo licha ya uchunguzi huo Taasisi hiyo pia
inachunguza vichwa vya malori 100 vinavyomilikiwa na mfanyabiashara
huyo.
Aidha
TAKUKURU pia inachunguza mikopo ya mfanyabiashara huyo ya zaidi ya Dola
za Marekani 3,000,000, sawa na Bilioni 6.3 za Kitanzania kutoka Benki
ya Barclays, pamoja na Dola 540,000 sawa na Bilion i 1.1 kutoka Benki ya
Equity.
Uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ukikamilika, mfanyabiashara huyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
No comments :
Post a Comment