Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka mawaziri wote pamoja na makatibu
katika wizara kuchukua likizo ya mapumziko ya lazima huku kukiwa na
taarifa za mabadiliko kwenye baraza la mawaziri.
Rais Kenyatta amesema kuwa mawaziri na makatibu watalazimika kushughulikia majukumu ya dharura.
Kwa
mujibu wa barua iliyotumwa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kiyua
likizo hiyo ya siku 11 itaanza Agosti 17 hadi agosti 28, mwaka huu
ambapo mawaziri hawatafanya ziara za kukagua miradi na mipango ya
serikali.
Likizo
hiyo ya mawaziri na makatibu inakuja huku kukiwa kuna taarifa kuhusu
Rais Kenyatta kuifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.
No comments :
Post a Comment