Sunday, August 16, 2020

VIJANA WAOMBA WADAU WA MAENDELEO KUTOA SEMINA VIJIJINI


Wanafunzi ,mafundi pamoja na wadau wa umeme nchini wakiwa katika semina ya vifaa vya umeme iliyotolewa na kampuni ya usambazaji na utengenezaji wa vifaa vya umeme nchini multicable (MCL) viwanja vya donbosco jijini Dar es salaam

       Na Khadija seif, Michuzi tv
MAFUNDI pamoja na wadau wa vifaa vya umeme waiomba serikali kuagiza makampuni ya vifaa vya umeme nchini kutoa semina Mara kwa Mara.

Akizungumza na Michuzi tv Jacob john ambae ni moja ya fundi umeme viwanja vya donbosco jijini Dar es salaam katika semina elekezi kuhusu vifaa vya umeme iliyotolewa na kampuni ya multicable (MCL) amesema wakati mwengine ni vizuri kupata ujuzi mpya pamoja na kuwafundisha vijana jinsi ya kujiajiri kupitia elimu ya ufundi.

"Kwa Sasa vijana wengi wameingia kwenye elimu ya ufundi ili kujikwamua kiuchumi hivyo kuwepo kwa semina Kama hizi zinasaidia mengi hasa kujifunza kuhusu vifaa vingi huku swala la kujiajiri likiwa linapewa kipaumbele kikubwa."

Pia amewaomba na wadau wengine kujitokeza kutoa elimu ya ufundi kwa sehemu mbalimbali hasa vijijini ili kuwanyanyua vijana .

Kwa upande wake Meneja masoko Denis Rungu ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuleta maendeleo chini ya Rais John Magufuli kwa kusisitiza swala la kuwepo viwanda chini.

" Serikali imejitahidi Sana kusitisha kuagiza nje cable na vifaa vingine vya miradi hapa chini ili viwanda vya ndani vikue na vithaminiwe."

Aidha, Rungu ameongeza kuwa mbali na viwanda kukua pia imekua ikiajiri vijana wengi hapa nchini.

Pia amesema tayari kampuni hiyo ya Mcl imeshasambaza vifaa vya kujenga miradi mikubwa kama vile flyover pamoja na madaraja mbalimbali.

 

No comments :

Post a Comment