Sunday, August 16, 2020

NSSF YATEKELEZA KWA VITENDO MAAGIZO YA JPM

Na MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amekiri utekelezwaji wa miradi ya kimkakati na maagizo mengine yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema Rais Dkt. Magufuli alitoa maagizo mawili katika mradi wa nyumba za NSSF uliopo Dungu; kwamba wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni waingie katika nyumba hizo agizo ambalo limeshatekelezwa na nyumba 99 ambazo zimekamilika tayari zimepangishwa.

Jenista alisema hayo baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Magufuli ambapo alianzia ujenzi wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, na kuongeza kuwa NSSF inafanya kazi nzuri na ina uwezo mkubwa unaoweza kusaidia uwekezaji.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Salimu Matimbwa, ambaye ni mmoja wa wapangaji wa nyumba za NSSF zilizopo Dungu, alisema amepata nyumba ambayo hakuitegemea kama angeweza kupata kwa sababu ni nzuri, imejengwa kisasa na inastahili kuishi binadamu yoyote.

Mkazi wa Kigamboni, Felix John, aliishukuru Serikali kupitia NSSF kwa sababu imewasaidia vijana kupata ajira katika mradi huo wa ujenzi barabara inayounganisha Daraja la Nyerere.
Naye Godfrey Kurumwa ambaye ni dereva Bodaboda ameipongeza Serikali pamoja na NSSF kwa kujenga barrabara pana ya kiwango cha lami

 Mjasiriamali Mwajuma Salumu Shukuru akiishukuru Serikali na NSSF, kwa kukamilisha ujenzi wa kipande cha barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni, na kuainisha kuwa kabla ya barabara hiyo ya lami walikuwa wanapata shida  kubwa ya vumbi. Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wikiMkazi wa Kigamboni, Meja Mstaafu wa JWTZ, Adiel Raphael Kaay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ubora wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,  kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF Balozi Ali Iddi Siwa

No comments :

Post a Comment