Waandishi wa Habari
wanachama wa DCPC wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka
NHIF baada ya kufunguliwa mkutano mkuu wa klabu hiyo mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF), Angela Mziray akizungumzia mbele
wa Waandishi wa Habari Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Jijini
Dar es Salaam (DCPC) wakati wa mkutano mkuu na uchaguzi mkuu wa
viongozi.
…………………………………………………
NA SULEIMAN MSUYA
ZIADI ya Watanzania
milioni 4.4 wananufaika na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), huku
mfuko ukisisitiza wananchi kujiunga kwa wingi.
Hayo yamesemwa na
Meneja Uhusiano wa NHIF, Anjela Mziray wakati wa mkutano mkuu na
uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari jijini Dar es
Salaam (DCPC) uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mziray alisema NHIF
ni chombo sahihi kwa usalama wa afya ya Watanzania hivyo anawaomba
waandishi kujiunga na kuhamasisha wananchi kujiunga kwa kuandika na
kuelezea faida za mfuko huo.
Alisema Watanzania
milioni 4.4 bado ni idadi ndogo hivyo wao wanaendelea kutoa elimu kwa
jamii kuhusu faida za mfuko huo kwenye maisha yao.
“Hadi sasa zaidi ya
Watanzania milioni 4.4 wananufaika na mfuko ila mikakati yetu ni idadi
hii iongezeke mara dufu hali ambayo itachochea ustahimilivu wa mfuko.
Ila nisisitize kuwa
NHIF ni sawa na kusema msaada tutani kwani imekuwa ikiwaokoa watu wengi
wakati wanapokutwa na majanga ya kiafya,” alisema Mziray.
Kwa upande wake
Meneja Masoko na Huduma wa NHIF, Hipoliti Lelo alisema mfuko huo
umefanyiwa mabadiliko mengi ili uweze kukidhihaja za wanufaika wore
ambao wanataka kujiunga wakiwemo waandishi wa habari.
“Tuna mifumo miwili
ya kunufaika na NHIF, wapo wanaochangia asilimia 6 ambapo mwajiri
anachangia asilimia 3 na mwajiriwa 3. Ila lipo kundi linalochangia
kuanzia 50,400, 100,000 hadi zaidi ya milioni 1 wote wananufaika na
mfuko na nyie waandishi tumewapa kifurushi maalum cha 100,000 ila
mmeshindwa kukichangamkia,” alisema.
Lelo aliwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuandika namna mfuko huo unavyoweza kumsaidia mtu katika wakati mgumu.
Meneja huyo aliwataka
waandishi kote nchini kutumia nafasi hiyo ya upendeleo kwa kujiunga na
mfuko huo ili waweze kukabiliana na changamoto za matibabu ambazo
wanaweza kukutana nazo.
Alisema fursa hiyo ya waandishi inawahusu wenza wao hivyo wanapaswa kuitumia kikamilifu.
Akizungumzia fursa
hiyo Mwandishi Mwandamizi, Salehe Mohammed alisema watahakikisha
wanaitumia kikamilifu ili waweze kukabiliana na changamoto za matibabu.
No comments :
Post a Comment