Monday, August 17, 2020

MPINA AWATAKA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO KUTAFUTA MASOKO YA UHAKIKA NA KUITUMIA VIZURI BANK YA MAENDELEO YA KILIMO


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia moja ya dawa za mifugo
katika kiwanda cha Farm Accesses Ltd cha mjini Arusha kinachotengeneza
pembejeo za mifugo. Waziri Mpina alitembelea kiwanda hicho jana akiwa
katika ziara ya kikazi
Waziri Luhaga Mpina, akiwa katika ziara ya kikazi  Mkoani Arusha na
Kilimanjaro aliambatana na wajumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya
Maendeleo ya Kilimo Bw. Japhet Justine (kushoto)

Waziri Luhaga Mpina katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro na Arusha

Msajili wa bodi ya nyama kutoka katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Bw.Imani Sichwale alikipongeza kiwanda cha Meat King kwa kuzalisha nyama
zilizo katika kiwango cha hali ya juu.

Na Mwandishi wetu, Arusha.


Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wawekezaji katika sekta ya
Mifugo husasani wamiliki wa viwanda vya nyama nchini kutafuta masoko ya
uhakika  ndani na nje ya nchi.

Waziri Mpina aliyasema hayo
jijini Arusha alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya  kutembelea


viwanda vya mazao ya mifugo ambapo alisema Serikali inawaunga mkono 
wawekezaji katika sekta ya nyama na kushauri wafanye upanuzi wa viwanda
vyao  kwani baada ya janga la covid 19 biashara sasa imeanza kurudi
vizuri.

“Changamkieni masoko na ziwepo products zote  katika masoko ya ndani watanzani na  wageni wanahitaji wazipate.”Alisisitiza.

Akiwa
katika kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat king mjini Arusha Mpina
aliwataka wafanye bidii katika kuhakikisha wanapata watu wanaoweza
kuyafikia  masoko kwa kwenda au kuwatumia mawakala hasa katika mikoa ya
Mwanza, Tanga na sehemu nyingine za nchi.

Katika ziara yake
kiwandani hapo Waziri Mpina, aliishauri Bank ya Maendeleo ya Kilimo TADB
kuangalia uwezekano wakupanua wigo wa mikopo ili viwanda viendelee 
kuwepo sambamba na kuinua soko la ndani na kuimarisha mnyonyoro wa
thamani  wanyama na kufanya bidhaa hizo ziwe na ushindani kimataifa,
kutoa ajira kwa watanzania na wafugaji wazidi kuinuliwa kiuchumi.

Akiongea
katika ziara hiyo ya Waziri Mpina, Kaimu Mkurugenzi wa mikopo na
biashara  kutoka Bank ya Maendeleo ya Kilimo Bw. Jeremiah Muhanda,
alisema Bank hiyo imeweza kuwasaidia wawekezaji kupata ,machine za
kisasa, mitaji yakufanyia kazi na kuwasaidia mitaji wafugaji kupitia
vikundi.

Na aliongeza kwa kusema kuwa Bank hiyo pia imewezesha
kiwanda cha pembejeo za mifugo cha farm access cha mjini Arusha mkopo wa
kiasi cha shilingi milioni mia nne tisini na tisa (499Milioni).

Kwa
upande wake Msajili wa Bodi ya nyama nchini Bw. Imani Sichalwe
alikipongeza  kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat King kwa kuzalisha
nyama yenye viwango vya juu ambapo awali ilikuwakiagizwa kutoka nje ya
nchi.

Alipokuwa katika kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh
Waziri  Mpina  alimpongeza muwekezaji huyo kwa kununua maziwa kwa
wafugaji kwa bei nzuri ya  shilingi mia nane themanini (880/-) kwa lita
ikiwemo kuwapongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuzalisha lita elfu nane
(8000) mpaka elfu tisa(9000)kwa siku na maziwa hayo kufika katika kila
maeneo nchini.

“Serikali itaendelea kuunga mkono na kusaidia
kutatua changamoto zozote na msipate  vikwazo kwenye soko zuri la
wafugaji wetu, ilikuweza kupata maziwa  mazuri na bora…Nawasihi pia
mpanue masoko kadiri mnavyoweza, nawahakikishia masoko yaliyopo
yataendelea kulindwa.” Alisema.

Aidha,Waziri Mpina alielekeza
bodi ya maziwa kufuatilia maziwa yanayoingizwa toka nje ya nchi kinyume
na utaratibu yaondolewe na walipe kodi za serikali na nchi isiwe dampo
la kuingiza bidhaa hizo kinyume nataratibu.

Alipotembelea kiwanda
cha nyama cha Elia Foods Overseas ltd kilichopo Wilayani 
Longido,Waziri Mpina  alimpongeza muwekezaji huyo kwa kufanya uamuzi wa
kujenga kiwanda hicho nchini.
 

Hata
hivyo muwekezaji huyo alimuomba Waziri Mpina kushugulikia changamoto
ya  kodi anayokabiliana nayo ili kuweza kuingiza vipuri toka nchi jirani
ya Kenya na  kuanza uzalishaji kwawakati, ambapo katika hilo Waziri
Mpina alielekeza dawati la  sekta binafsi la wizara yake kushughulikia
changamoto hiyo mara moja ili uzalishaji katika kiwanda hicho uanze.

Ziara
ya Waziri Mpina Mkoani Arusha ilihusisha kiwanda cha kuchakata nyama
cha  Meat King, Elia Foods Overseas ltdnakiwanda cha maziwa cha
Kilimanjaro Fresh.

 

No comments :

Post a Comment