Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akisalimiana na Afisa Mkuuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Severine Lalika.
Sehemu ya wageni waalikwa
……………………………………
Benki ya NMB imewahimiza wafanyabiashara nchini kujiunga na
Mtandao wa
Akizungumza jijini Mwanza juzi
katika wa mkutano wa mtandao huo wa Kanda ya Ziwa, Afisa Mkuu wa Wateja
Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi alisema wafanyabiashara
wanaojiunga na mtandao huo pia hupata fursa kukutana na kujadiliana ana
kwa ana na uongozi wa juu wa benki hiyo.
“Kupitia vikao vya kila mwaka vya NMB Business Executive
Network wafanyabishara hupata elimu kutoka kwa wataalam wa fani
mbalimbali kuhusu namna bora ya kufanya biashara kirahisi, kwa tija na
gharama nafuu kupitia teknolojia,” alisema Mponzi
Mtandao huo ulioanza mwaka 2014,
tayari unajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 760 kutoka miji ya Dar es
Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Mtwara na Morogoro.
“Hata wafanyabiashara wasiyo wateja wa NMB wanaweza kujiunga na
mtandao huu kuona fursa, bidhaa na huduma zinazotolewa na benki yetu
inayoongoza kwa faida baada ya kodi na ubora kwa miaka 11 mfululizo,”
aliongezea Mponzi
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB – Alex Mgeni aliwataka
wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma ya bima
inayotolewa na benki hiyo ili kupata fidia kwa haraka na wakati kupitia
matawi zaidi ya 220 nchini.
“Tayari tumezindua huduma ya bima za aina mbalimbali ikiwemo ya
mazao ya kilimo itakayowawezesha wakulima kupata fidia ya madhara na
uharibifu unaotkana na majanga kama mafuriko, ukame, uharibifu wa wadudu
na ndege waharibifu,” alisema Mgeni
Naibu wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.
Angelina Mabula aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo aliipongeza
benki hiyo kwa kuanzisha bima ya mazao ya kilimo na kuutaka uongozi
kuongeza kasi ya elimu kwa umma kuhusu bidhaa na huduma hiyo. “Bima ya
mazao itanufaisha na kuongeza tija katika sekta ya kilimo ambayo
mnyororo wake wa thamani unahusisha zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania.
NMB endeleeni kuelimisha umma kuhusu huduma na bidhaa,” alisema Dk
Mabula
No comments :
Post a Comment