Monday, August 17, 2020

SHIRIKA LA WORLD VISION WAKABIDHI MRADI WA MAJI HANDENI WENYE THAMANI YA MILIONI 199.1


MKUU wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila akikata utepe kuashiria uzindua mradi wa maji

mradi wa maji uliojengwa na shirika la World vision hongkong na kusimamiwa na word vision Tanzania katika Kijiji cha Pozo
Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani
ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaika wananchi 1,709

 

MKUU wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila akionya maji hayo mara baada ya kufanya uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa na shirika la World vision hongkong na kusimamiwa na word vision Tanzania katika Kijiji cha Pozo
Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani
ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaika wananchi 1,709

Mkuu wa wilaya
ya
Handeni Toba Nguvila kulia amtwisha ndoo ya maji kichwani mkazi wa
Kijiji cha Pozo Mwanahamisi Selemani  mara baada ya kuzindua mradi
wa maji

radi wa maji uliojengwa na shirika la World vision hongkong na kusimamiwa na word vision Tanzania katika Kijiji cha Pozo
Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani
ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaika wananchi 1,709

MKUU wa wilaya ya Hanadeni Toba Nguvila kushoto akimpongeza Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision
Tanzania Jackline Kaihura wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji

MKUU
wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mradi wa maji wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi
wa Shirika la World Vision
Tanzania Jackline Kaihura

Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision
Tanzania Jackline Kaihura akisoma taarifa yake kabla ya uzinduzi wa mradi huo
       

 

SHIRIKA la World
Vision Tanzania limekabidhi mradi wa maji uliojengwa katika Kijiji cha Pozo
Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani
ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaisha wakazi wa kaya 582 ambayo ni sawa
na wanufaika 1,709.

Makabidhiano hayo
yalifanywa na Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision
Tanzania Jackline Kaihura kwa Mkuu wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila katika
Kijiji cha Pozo.

Alisema kwamba mradi huo wa maji katika Jijiji
cha Pozo umetekelezwa kwa ufadhili World Vision Hongkong chini ya usimamizi wa
shirika la World Vision Tanzania Kwamsisi AP katika mwaka wa fedha 2018/2019
kwa ushirikiano na wataalamu wa maji katika Halmashauri ya Handeni (Ruwasa)

Akizungumza mara
baada ya makabidhiano hayo Jackline alisema kwamba mradi huo umetekelezwa na
wakandarasi watano ambapo Victoria Drilling Company walichimba kisima kwa kiasi
cha milioni 28, 137, 100, Kisomboko Builders Limited walifanya ununuzi na
usambazaji wa mabomba kwa kiasi cha milioni 30,500,000.

Alimtaja mkandarasi
mwengine kuwa ni Siha Enterprises Limted ambao walifanya kazi ya ujenzi wa
tenki na vituo vya kusambaza maji (DPs) wenye thamani ya milioni 62, 260, 670,
Kiroi Construction Limted ambao walitengeneza kibanda cha pump chenye thamani
ya milioni 15,891,296.

“Lakini wakandarasi
wengine ni  Best one Limited ambao
walifanya ununuzi na uwekaji wa solar Panels kwa kutumia kiasi cha milioni
58,642,460 huku ununuzi wa pump ambao ulifanywa na worldvision ukigharimu kiasi
cha milioni 3,570,450”Alisema

Aidha alimueleza Mkuu
huyo wa wilaya kwamba ipo miradi mingine ya maji iliyotekelezwa kwa ufadhili wa
shirika la worldvision chini ya Kwamsisi Area Program ambayo imekamilika mwaka
huu na yote imekamilika kwa mafanikio.

Alisema ni mradi wa maji wa Kijiji cha Kwanyanje ambao uligharimu jumla ya fedha za kitanzania
sh.milioni 141, 84,785.76 na mradi wa kukarabati miundombinu ya maji kijiji cha
Kwasunga uliogharimu kiasi cha milioni 150,834,540.

“Pia kuna mradi wa maji unaohudumia vijiji vya Kwamsisi na Kwedikabu ambao ulikamilika mwaka 2018
na tayari umewanufaisha wananchi wa vijiji hivyo na wanauendesha wenyewe kwa
kupitia vyombo vya watumia maji ambao uligharimu kiasi cha milioni 207.

Awali akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo Mkuu wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila alisema
ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo kuanzia hatua ya tenki, koki na maeneo ya kuchotea maji yapo vizuri huku akilishukuru shirika hilo kwa kusaidia juhudi
za serikali katika kusaidia kuipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Alisema wananchi hao walikuwa wanakunywa maji ya kwenye mabwawa na madimbwi ambayo sio salama kwa
afya zao na watoto lakini hivi sasa wakwenda kunywa maji salama yaliyochimbwa kwenye kisima chini ya ufadhi wa Shirika la Wordvision Hongkong wakiwa ni wadau
muhimu wa maendeleo kwenye wilaya ya Handeni na hapo Pozo.

“Mradi huu mmeupata ni mzuri na maji ni safi na salama hivyo niwapongeze world vision na wataalamu wa Ruwasa. Lakini wananchi mhakikishe mnaulinda na kuutunza kama mboni ya jicho”Alisema

Hata hivyo alisema ni muhimu mradi huo utunzwe ili uweze kuwanufaisha leo na siku zijazo huku akieleza wakiona watu wanafanya uharibifu viongozi wachukue hatua kali kwa
faida ya wananchi wa eneo hilo.

No comments :

Post a Comment