Saturday, August 1, 2020

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA BoT, NANENANE SIMIYU


 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto), akimsikiliza Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT, Bi. Vicky Msina (katikati) huku Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Bernard Kibesse (kulia) akishuhudia wakati Kiongozi huyo alipotembelea banda la Benki Kuu kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo nya mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambako maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu wa 2020 yanafanyika. Makamu wa Rais alitarajiwa kufungua rasmi maonesho hayo.
 Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Zalia Mbeo (kushoto) akimuongoza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kutembelea banda hilo.
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akipokea mfuko wenye machapisho mbalimbali yanayoelezea shughuli za BoT kutoka kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Kibesse wakati alipotembelea banda hilo leo Agosti 1, 2020
Makamu wa Rais akiondoka wkenye banda la BoT baada ya kulitembelea.
 
NA
KHALFAN SAID, NYAKABINDI
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea
banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo
ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ambako kiongozi huyo amefika kufungua rasmi
maonesho ya mwaka huu ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja hivyo.
Makamu
wa Rais alipokewa na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Y. Kibesse na
Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Zalia Mbeo ambapo alitembelea idara
mbalimbali za Benki hiyo na kuelezwa jinsi zinavyowahudumia wananchi wanaofika
kwenye banda hilo.
Maonesho
ya mwaka huu ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020.”
Lengo
hasa la maonesho hayo yanayofanyika kitaifa kwa mara ya tatu mfululizo kwenye
viwanja hivyo ni kutoa fursa kwa Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika
kuona na kujifunza matumizi ya teknolojia Bora za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa
ajili ya kuongeza tija na uhakika wa chakula, kukidhi mahitaji ya viwanda na
masoko.

No comments :

Post a Comment