Rania Nasser ambaye ni
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano ameandaa maonyesho ya picha yanayojulikana
kama ‘Watu wa Tanzania’ ambayo yatafanyika Alliance Francaise jijini
Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Agosti 2020.
Matumizi ya picha na video
kuelezea stori au hadithi ni muhimu Sana, yanaelimisha, kubadilisha
Habari za kihadithiwa na muonekano pamoja na kuleta mabadiliko chanya
kwa Dunia. Tumeona mfano mingi kwenye hili. Mabadiliko yanaanza kwa
kubadilisha maono ya jamii.
Tangu akiwa na umri mdogo, Rania
ametembelea sehemu mbali mbali za nchi yake Tanzania na sehemu zote
hizo ambazo ametembelea na watu aliokutana nao, na Habari zile ambazo
amezipata, ameona kilicho bora kwa Watanzania.
Rania pia ameweza kutembelea nchi zingine ulimwenguni lakini ukarimu na upole wa Watanzania umekuwa ni wa kipekee.
Wakati wa kutembelea nchi hizo
zingine, Rania ametengeneza marafiki wengi. Kitu kimoja ambacho ameweza
kutambua ni kwamba wengi wanajua machache kuhusu Bara la Afrika, na Sana
Sana Tanzania. Anasema ‘naelewa ya kwamba kuna watu hawajui ya kwamba
Afrika sio nchi, na hii sio kwa kila mtu, siwezi kupata picha kwa
umasikini unaokumba vijiji vyetu, mapigano kwenye Miji yetu, magonjwa na
mengine mengi’
No comments :
Post a Comment