****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA)
wameelekezwa kufikia mwezi Oktoba mwaka huu
kumalizika kwa jengo la
kuhifadhi mtambo wa kupima mita za umeme kwani mpaka sasa taratibu za
manunuzi umeshaanza kufanyika.
Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe baada ya kutembelea
kituo hicho kilichopo Misugusugu Mkoa wa Pwani.
Akizungumza katika kituo hicho
Prof.Shemdoe amewataka WMA washirikiane na Tanesco pamoja na TPDC ili
kuweza kufanikisha jambo la kupima mita zinazoweza kutumika katika
matumizi.
“WMA wameanza mkakati wa kupima
mita za umeme, niombe suala hili lifanyiwe kazi kwa haraka lile jengo
ambalo linatakiwa lijengwe kwaajili ya kuhifadhi mtambo wa kupima mita
za umeme lijenge na ikiwezekani kabla ya mwisho wa mwaka huu”. Amesema
Prof.Shemdoe.
Aidha Prof.Shemdoe ameomba kuanza
mchakato wa kupata mtambo mwingine ambao utasaidia kupima mita za gesi
zinazotumika viwandani na pengine ambazo tumeanza kuzitumia majumbani
ili waweze kulipa kutokana na matumizi sahihi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
Mkuu-WMA, Dkt.Ludovick Manege amesema utaratibu wa kuwepo kwa mtambo wa
kupima mita za umeme umeshaanza na hata hivyo kufikia mwishoni mwa mwaka
huu utakuwa tayari umeshakamilika.
“Pamoja na sasa tunapima dira za
maji lakini kwa kufikia mwezi wa kumi tutakuwa tumeanza kupima dira za
umeme kwasababu tayari taratibu za manunuzi zimekamilika”.Amesema
Dkt.Manega.
No comments :
Post a Comment