Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra
Oswald (wa pili kushoto ) pamoja na Msaidizi wa Mipango Vodacom Tanzania
Foundation, Kelvin Boya wakiwaelezea wateja kuhusu huduma ya Instant
School walipotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44 ya
biashara ya kimataifa ya sabasaba
Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi, Amina Salum Ali
akimkabidhi Tuzo ya Banda bora la sekta ya Mawasiliano na Tehama kwenye
maonesho ya 44 ya kimataifa ya biashara (Sabasaba) Meneja wa mauzo wa
Vodacom Tanzania PLC, kanda ya Temeke, Angetile Martin. Vodacom iliibuka
mshindi wa kwanza katika kipengele hicho baada ya kuonesha vitu
mbalimbali ikiwemo robot anayeitwa Pepper.
Baadhi
ya wateja waliotembelea banda letu, wakizungumza na robot aitwaye
Pepper kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni yetu wakati wa
maonesho ya sabasaba.
No comments :
Post a Comment