Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya ( aliyevaa shati la blu) akitazama aina ya mpunga
wakati alipotembelea kituo cha ununuzi wa mpunga unaofanywa na NFRA
kanda ya Makambako katika kijiji cha Uturo wilaya ya Mbarali leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya akiwa ndani ya ghala la kuhifadhia mpunga wa wakulima
wa kijiji cha Uturo wilaya ya Mbarali alipotembelea kukagua msimu wa
ununuzi unaofanywa na NFRA.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya akiwa anakagua mfuko unaotumika kuhifadhia mpunga
katika kituo cha manunuzi Uturo wilaya ya Mbarali leo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akitazama mche bora wa muembe wakati
alipotembelea chuo cha Mafunzo ya Kilimo na Mifugo ( MAMRE) wilaya ya
Wanging’ombe leo
Wanachuo wa chuo cha Mafunzo ya
Kilimo Igurusi wilaya ya Mbarali wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( suti ya blu katikati) mara
baada ya kumaliza mazungumzo wanafunzi hao leo
-Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akitazama wanyama kazi aina ya
punda wanaotumika kufundishia wanafunzi katika chuo cha Kilimo na Mifugo
( MAMRE) mkoani Njombe leo.
…………………………………………….
Wakulima nchini wamehakikishiwa
kuwa serikali itaendelea kununua mazao yao kwa ajili ya
kuongeza hifadhi
ya kutosha ili kuwa na uhakika na usalama wa chakula nchini.
Kauli hii ya serikali imetolewa
leo wilayani Mbalali na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya
wakati alipotembelea kituo cha ununuzi zao la mpunga kijiji cha Uturo
unaofanywa na Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA) kanda ya
Makambako
“Serikali kupitia wizara ya Kilimo
itaendelea kununua mazao ya wakulima hususan mahindi na mpunga kwa
wingi hivyo wakulima msidanganywe kuwa muda umebaki mfupi wa kupeleka
mazao yenu NFRA. Leteni hapa mpunga wenu tutaununua wote” alisema
Kusaya.
Akiwa katika ghala la Ushirika
Uturo Mbarali Katibu Mkuu huyo aliongea na wakulima wa mpunga na
kuwahakikishia kuwa wizara imejipanga kuona nchi inaendelea kuwa na
usalama wa chakula ndio maana anapita mikoani kujionea hali ya
uzalishaji mazao
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makambako Frank Felix
alisema tayari wakala umeshanunua tani 1,700 za mpunga kati ya malengo
ya tani 5,000 na mahindi tani 2,933.174 kati 25,000 msimu huu.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima
wa mpunga Mbarali Said Nkenja alishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa
kununua mpunga kwani umesaidia kuongeza ushindani wa bei sokoni.
“Tunamshukuru sana Rais Dkt.John
Pombe Magufuli kwa uongozi wake unaowajali wakulima nchin.Leo Mbarali
tunafurahia kuuza mpunga kwa NFRA tena bei ni nzuri .Tunaomba iendelee
kununua zaidi mpunga upo mwingi tunavuna bado” alisema mkulima Said
Nkenja.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu
Kusaya alitembelea Chuo cha mafunzo ya Kilimo na Mifugo ( MAMRE) cha
Wanging’ombe mkoani Njombe na kutoa agizo kuwa wanafunzi wanaoshindwa
kulipa ada ya mafunzo wasifukuze badala yake utafutwe utaratibu rafiki.
Kusaya alitoa agizo hilo kufuatia
malalamiko ya wanafunzi kusema baadhi yao wameshindwa kuendelea na
masomo baada ya kushindwa kulipa ada na michango mingine.
“Vyuo vyote 29 ( 14 vya serikali
na 15 vya binafsi) ni vyangu kwani vinalenga kuzalisha maafisa ugani
watakaokwenda kuhudumia wakulima nchini.Nitaendelela kuvisaidia bila
kuangalia nani anakimiliki muhimu vitoe mafunzo bora kwa wanafunzi wa
kitanzania” alisema Kusaya.
Kusaya aliusihi uongozi wa chuo
cha MAMRE kutafuta njia rafiki kuwasaidia wanafunzi wenye mazingira
magumu yanayosababisha kutolipa ada kwa muda.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo
ameahidi kutoa kompyuta ili kuwezesha kuanzisha maktaba mtandao ( e-
learning) na kugharimia mwanafunzi mmoja kwenda kujifunza kanuni bora za
ufugaji kuku kisasa katika vhuo cha Ihemi Iringa kwa gharama za
serikali.
Katibu Mkuu amesema katika
kuboresha mafunzo kwa vitendo atakipatia Chuo hicho Kitalu nyumba moja
(Green House) ili wafundishe klimo cha mbogamboga na matunda (
horticulture).
Chuo cha MAMRE kina wanafunzi 103 wa ngazi ya astashahada na stashahada.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo
hicho Geofrey Mapesa alisema changamoto kubwa Kwa sasa ni kukosekana
kwa mfumo wa udahili wa pamoja ( Central Admission System) hali
inayopelekea upungufu wa wanafunzi.
Tayari wanafunzi 169 wamehitimu
mafunzo ya kilimo na mifugo tangu chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 2014
chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe
No comments :
Post a Comment