Mkurugenzi wa Kiwanda
Cha Transfoma Zahir Salahe,akitoa maelezo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji Angellah Kairuki,Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Kenani Kihongosi,na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa TIC Saudi
Riganda.
Mkurugenzi wa Kiwanda
Cha Transfoma Tanelec Zahir Saleh akiwa na waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki wakati alipofanya ziara ya kukagua
kiwanda hicho na kuzungumza na Mwekezaji huyo
Waziri wa nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi
wa Tanelec Zahir Saleh pembeni Ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Kenani
Kihongosi.(Picha na Ashura Mohamed)
………………………………………………………………………
Na.Mwandishi Wetu – Arusha
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji,Angellah Kairuki amesema kuwa serikali ya Awamu
ya Tano,inaendelea kutengeneza Mazingira mazuri kwaajili ya Uwekezaji
ili kuvutia sekta hiyo.
Akizungumza jijini
Arusha katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili Kairuki alisema kuwa
serikali chini ya raisi Daktari John Pombe Magufuli inaendelea
kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi ili Wawekezaji waendelee kutumia
fursa Mbali mbali.
Akizungumza katika
kiwanda Cha Kutengeneza Transfoma Cha Tanelec amewapongeza kwa kazi
nzuri ambayo wanaifanya na kuwataka kuendelea kuongeza jitihada na
kuhakikisha kuwa wanatumia malighafi za ndani ya nchi.
“Kiwanda Hiki Cha
Tanalec Ni kiwanda kikubwa Sana,na kimeweza kuitangaza nchi katika bara
la Afrika Ila niwaombe kuwa zipo malighafi ambazo mnaagiza nje ya nchi
Sasa tujaribu kuhakikisha kuwa tunawasiliana na viwanda vingine kuona
namna ya kupata Mali ghafi hapa hapa nchini,tuokoe hizo fedha za
kigeni”alisema Kairuki
Alisema kampuni hiyo
ambayo ni mbia na serikali inajitahidi kuhakikisha inatengeneza
transfoma nyingi kwaajili ya kuwezesha Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) kusambaza umeme hadi kufikia Juni 29 mwaka huu serikali ya
awamu ya tano imefanikisha kusambaza umeme kwa vijiji 9,314
ikilinganishwa na vijiji 2018 vilivyokuwa vimeunganishwa umeme kwa mwaka
2018 sawa na ongezeko la asilimia 361.5 kupitia mpango kabambe wa
usmbazaji umeme vijijini
Alisema tangu Rais
Magufuli alipoingia madarakani hadi leo hii wateja zaidi ya milioni 2.7
wamepata umeme sawa na ongezeko la asilimia 361.5 huku akiwasisitiza
kuendelea kufanya tafiti za kimasoko ili kuona uhitaji wa transfoma
mbalimbali katika nchi za EAC pamoja na nchi nyingine.
“Nawapongeza kwa
kuzalisha transfoma hizi lakini endeleeni kuendelea kutengeneza
transfoma na kupata masoko zaidi katika nchi za EAC pia fanyeni tafiti
zaidi za masoko ili kuuza zaidi transfoma hizi zinazozalishwa Tanzania “
Mkurugenzi wa
Tanelec, Zahir Saleh alisema kuwa wanalazimika kununua waya aina ya
enamael kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ingawa Tanzania kuna
viwanda vinne vinavyotengeneza waya ila hawatengenezi waya aina hiyo
ndio maana wanaagiza nje ya nchi.
Pia aliomba Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) kuondoa urasimu wa kodi mbalimbali pale
wanapoingiza bidhaa kutoka nje y nchi kwaajili ya kutengeneza transfoma
nchini ni kuishukuru serikali kushirikiana kwa pamoja katika kuendesha
kiwanda hicho kwani hivi sasa tangu kuanzishwa kwa viwanda vingi awamu
hii ya tano wamiliki wa viwanda mbalimbali vilivyopo nchini wanaona
mafanikio.
Naye Mkuu wa Wilaya
ya Arusha, Kenani Kihongosi alimshukuru uwepo wa kiwanda hicho ikiwemo
kusambaza transfoma zaidi katika miradi mbalimbali Rea iliyopo vijiji
mbalimbali nchini na mijini.
Kenani alitumia muda
huo kuwakaribisha Wawekezaji wote Wilaya Arusha na kusema kuwa Serikali
mkoani Arusha bado itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za
kuhakikisha viwanda vinaongezeka ili kuongeza Ajira.
No comments :
Post a Comment