Naibu Waziri wa
Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu, akitoa hotuba ya
ufunguzi wakati wa hafla fupi ya kutoa Nyota kwa Hoteli za Mkoa wa
Dodoma zilizopangwa katika Daraja za Ubora.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii mhe. Constantine Kanyasu akimkabidi Nyota tatu (3)
kwa Kaimu Meneja wa Nashera Hotel Ms. Epiphania Ponera kwenye halfa ya
utoaji Nyota kwa hoteli zilizokidhi vigezo
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda akizungumza kwenye hafla ya
utoaji Nyota kwenye hoteli zilizokidhi vigezo iliyofanyika Jijini
Dodoma
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na baadhi ya viongozi
na watumishi wa Idara ya Utalii kwenye picha ya pamoja leo katika hafla
ya utoaji nyota katika Hoteli zilizokidhi vigezo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Maliasili na
Utalii leo katika hafla ya utoaji nyota katika Hoteli zilizokidhi vigezo
vya ubora iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
SERIKALI imewataka
Wawekezaji nchini kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Hoteli zenye nyota
nne ama tano kutokana na kutokuwepo katika Jiji la Dodoma
Hatua hiyo imekuja
kufuatia Serikali kuzitangaza hoteli tatu pekee ndizo zenye nyota tatu
za Jijini Dodoma ambazo ni Fantacy Village,Nashera Hoteli na New Dodoma
Hoteli.
Hayo yamesemwa leo
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
katika hafla ya kutoa daraja za nyota kwa hoteli zilizopangwa katika
daraja za ubora za Jijini Dodoma.
Mhe.Kanyasu amesema
licha ya Jiji la Dodoma kuwa ndio makao makuu ya Serikali lakini bado
kuna mahitaji ya hoteli zenye nyota nne na tano hivyo amewataka
wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo kwa kujenga hoteli zenye ubora.
“Wito wangu hatuna
hoteli zenye nyota nne na tano hapa Dodoma,niwaombe Wawekezaji
kuchangamkia fursa hii,kutafuta maeneo kwani Jiji la Dodoma linatoa na
maeneo hayo yapo,”alisema.
Amesema uwepo wa
hoteli nzuri kutachangia kuwafanya watalii ambao huja nchini kufikia
katika maeneo yenye ubora hivyo kuliongezea Taifa mapato.
“Hitaji la wageni ni
malazi na huduma bora hivyo upangaji wa madaraja ni jambo muhimu ,wito
wangu kwa wamiliki wa hoteli kuwa na lugha nzuri kwa wageni ambao
wanawapokea,”alisema.
Aidha, Mhe.Kanyasu
amesema changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo ni hoteli kujengwa
sehemu ambazo sio sahihi pamoja na kuwepo kwa wafanyakazi ambao hawana
sifa.
“Niwaombe wamiliki wa
hoteli ambazo tumezikagua na kukuta hazijakidhi vigezo kuliangalia kwa
umakini jambo hili kwa kujenga sehemu sahihi pamoja na kuchagua
wafanyakazi wenye sifa,”alisema.
Kwa upande
wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof. Adolf Mkenda
amesema zoezi la kupanga madaraja ya nyota kwa hoteli lilianza katika
Mikoa ya Dar es salaa,Pwani,Arusha,Mara na sasa Dodoma.
Amesema lengo la
zoezi hilo ni kubaini ubora wa hoteli ili kuwasaidia Watanzania pamoja
na wageni ambao wanatoka nje ya Tanzania kujua ni sehemu gani wanatakiwa
kufikia pindi wanapokuja nchini na kujua ubora wa hoteli.
Amesema wameanzisha Mfumo wa Kieletroniki ambao utakuwa ukiwawezesha wamiliki wa hoteli kupima ubora wa hoteli zao.
Prof.Mkenda amesema kwa Jiji la Dodoma walikagua,hoteli,nyumba za wageni 428 ambapo walizokuta zenye ubora ni 24 pekee.
Naye, Mtaalamu
watathmini wa Ubora wa Hoteli,Hassan Rehani amesema wamekuwa wakitoa
nyota za hoteli kutokana na kujaza madodoso ambayo baadae huangalia
ubora,pamoja na kutumia vigezo tisa ikiwemo kuwepo kwa vifaa vya kuzuia
majanga.
“Changamoto ambazo
tumekuwa tukikutana nazo kwanza ni kutokupewa ushirikiano kutokana na
wengi kujua sisi ni askari,wafanyakazi kuwa na uwezo mdogo pamoja na
kutokuwepo kwa wahusika pindi wanapokuwa wakiwahitaji,”amesema.
No comments :
Post a Comment