Baadhi ya wateja wa TTCL (kushoto) wakipata huduma za usajili laini zao walipotembelea Banda la TTCL katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba. |
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limepeleka huduma yake maarufu ya ‘T-Burudani’ katika Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limepeleka huduma yake maarufu ya ‘T-Burudani’ katika Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi ndani ya Banda la TTCL, Meneja Uhusiano wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania, Bi. Puyo Nzalayaimisi alisema Watanzania
watakaotembelea maonesho ya mwaka huu ndani ya banda lao, watajipatia
huduma ya T-Burudani nyenye ofa ambayo inatamwezesha mteja kupakua,
kuhifadhi pamoja na kuangalia filamu aipendayo hata bila ya kuwa na
mtandao wa intaneti.
Aliwaomba wananchi hasa wapenzi
wa filamu nchini kufurahia ofa hiyo ya shilingi 2000 tu na kujipatia
huduma ya T-Burudani toka TTCL itakayomwezesha mteja kuangalia filamu na
tamthilia aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti.
Mfanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Emerco Mashelle (kulia) akimuhudumia mmoja wa wateja wa TTCL waliotembelea Banda lao katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
“Huduma ya T-Burudani ya TTCL ni
rahisi inamuwezesha mteja kupakua filamu bila kutumia kifurushi cha
intaneti, mteja ataweza kuangalia filamu zote za ndani ya nchi pamoja na
kimataifa, mteja ataweza kupakua kupitia simu janja ya mkononi pamoja
na kompyuta ya kiganjani ‘Tablet’,” alisema Bi. Nzalayaimisi.
Aidha akifafanua zaidi juu ya
huduma hiyo, alisema TTCL imeweka mfumo rahisi utakaomuwezesha, mteja
kupakua filamu aitakayo kutokana na maudhui anuai duniani ikiwa ni
pamoja na Hollywood, Nollywood, Bollywood, HBO, na Bongo movies.
Aliongeza huduma nyingine ambazo
TTCL inazitoa katika viwanja vya Sabasaba ni pamoja na huduma za usajili
laini kwa wateja, kurudisha laini zilizopotea,vifaa vya internet kama
modem na vinginevyo, huduma za T-PESA, huduma za mkongo wa taifa wa
mawasiliano na huduma za Data Senta.
Kushoto ni mmoja wa wateja akihudumiwa ndani ya banda la TTCL katika Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
No comments :
Post a Comment